Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, February 23, 2026

WATU MASHUHURI WALIOSHIRIKI MAZISHI YA BABA MZAZI WA BEKI WA SIMBA.

 

Beki wa Simba Abdulrazack Spear Hamza mwenye Flana nyeusi [kulia] akizungumza na ndugu na jamaa waliomkimbilia kwenye msiba huo mzito wa Mpendwa baba yake hayati Spear Mohamed Hamza.

Mansoor Chamchua ‘Mzee wa Bums’ambaye ni Swahiba Mkubwa wa Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania’TFF’ Wales Karia, akisalimiana na Faudhi Al-Saed ‘Maarufu Micho’ambaye baba yake mzazi ndiye Mmiliki wa mabasi ya Kampuni ya Al-Saed.

Faudhi Micho akimtania Mpiga picha wa Mtandao baada ya kumshuhudia akiwaphotoa picha hizi.

Shehe Omar Ally ambaye ni Mhadhini Mkuu wa Msikiti Mkuu wa Morogoro ambaye pia ni Mshauri wa Mufti, ndiye aliyetoa mawaidha kwenye msiba huo.

Geofrey Job Maarufu Jofu Job[kulia] mwenye kofia] ambaye ni baba mdogo wa beki kisiki wa Yanga Dickson Nickson Job akibadilishana mawazo na Mhe diwani wa Kata ya Saba saba Mohamed Lukwele[kati] ambaye baraza la madiwani lililopita alikuwa Naibu Meya, kushoto anayezungumza ni Mlapakolo.

Shehe Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Shehe Jafar Sineli

 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro Nickson Mkilanya[kulia] akiwa msibani hapo na Diwani wa Kata ya Kihonda Maghorofani Mhandisi  Hamis Ndwata ambaye pia ni mmoja wa Madiwani waliogombea kiti cha Umeya wa Halmashauri ya Mji wa Morogoro laki kura hazikutoka na nafasi hiyo kunyakuliwa na Khalid Matengo diwani wa kata ya Mji Mkuu.

Shabiki Maarufu wa Simba Mkoa wa Morogoro Hussen Kilimo anayefanya shughuri za kusafisha viatu jirani na mzunguko wa barabara uliopo katikati ya Mji wa Morogoro jirani na stend ya zamani ya daladala ambayo kwa sasa imegeuzwa kuwa maegesho ya magari naye alikuwepomsibani hapo.


 

Gari lililobeba mwili wa hayari Spear likikatiza katikati ya uwanja kuelekea makaburi ya Magadu nje kidogo ya Mji wa Morogoro.

Abdulrazack alianza kuibua kipaji chake cha soka kwenye uwanja huu, kauli hii aliitoa hayati Spear alipohojiwa na Mtandao huu enzi za uhai wake.

No comments:

Post a Comment

MAJAJI 2 WAHUDHURIA IBADA YA KUMUOMBEA KIGOGO WA SUA MAREHEMU DKT MBILU.

         Mchungaji Dkt Rhoda Chamshama akiongoza ibada hiyo Katibu Mkuu wa  KKKT Usharika wa Mji Mpya Mshana akimuaga Mzee wake wa kanisa S...