Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, February 9, 2026

VITUKO VYA USHWAHIRINI.


 

     JANA kwenye Pilika pilika zangu za kusaka matukio Mtaani nimekutana na kichekesho hichi.

Kweli nimeamini ‘Mchafu hachafuki ’

Dada mmoja ambaye amejibana bana akiweka starehe kando akapambana na kufanikiwa kujenga nyumba ya nyumba vitatu hvi karibuani akahamia kwenye mjengo wake.

 

Kufuatia hali hiyo amejikuta hata asimu anaytumia ameradhimika kuikopa kwenye makampuni ya simu huku  akitakiwa kulipa shilingi elfu Moja kila siku mpaka deni hilo litakaptamatika.

 

Mashariti ya Mkopo huo usipoingiza kiasi hicho cha pesa wahusika wakanata mawasiliano ukilipa deni simu inarejea hewani.

 

Juzi kati dada huyo hakufanikiwa kuli deni hilo na simu yake ikazimwa, jirani yake ambaye anaishi nyumba ya kupanga huku akimiliki simu ya bei mbaya[sio ya mkopo]

 

Dada huyo anayeishi nyumba ya kupanga akapaza sauti akimfumbia mafumbo jirani yake huyo akimwambia.

 

“Shoga yangu jana kutwa nzima nimekupigia simu hukupatikana hiyo ni hadha ya hizo simu za mkopo.pambana shogaangu kwa urembo wako sio mtu wa milimiki simu ya Mkopo”

 

Kauli hiyo ilimkera dada mkopa simu ambaye naye alimjibu hivi.

 

.”Ni heri mimi niliye kopa simu lakini nalala kwangu je wewe unamiliki simu ya laki tano halafu unalala kwenye nyumba ya kupanga.

 

 Kweli kwa mwezi mimi nalipa deni la simu elfu 30 na hii ni kwa muda flani namaliza deni wewe kila mwenzi unalipa kodi ya nyumba laki Moja na unafanya hivyo kila Mwaka na Umri ndio huo unasonga mbele ukifuzwa kwenye hiyo nyumba naomba ulale kwenye hiyo simu yako ya laki 5”

Kwenye kisa hichi mjanja ni nani na Mjinga ni nani?

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MAJAJI 2 WAHUDHURIA IBADA YA KUMUOMBEA KIGOGO WA SUA MAREHEMU DKT MBILU.

         Mchungaji Dkt Rhoda Chamshama akiongoza ibada hiyo Katibu Mkuu wa  KKKT Usharika wa Mji Mpya Mshana akimuaga Mzee wake wa kanisa S...