Mzee Mahita akishiriki kupokea dua la kumuombea Mpendwa wetu
Kama
unavyoonekana pichani Mzee Mahita akisaidiwa kutembea na Hassan Malingo
diwani wa zamani wa kata ya Mji Mkuu.kuelekea kwenye gari lake tayari
kwa safari ya kwenda makaburi ya Kolla kushiriki mazishi ya Spear.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
MKUU wa Jeshi la Polisi Nchini I.G.P Mstaafu Alhaji Omari Idd Mahita jana amewaongoza Mamia ya wananchi wa Mkoa wa Morogoro kumzika Spear Mohamed Hamza ambaye ni baba mzazi wa beki kisiki wa Simba Abdulrazack Spear Hamza.
Hayati Spear ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu mbali mbali za mkoani Morogoro amefariki juzi na kuzikwa jana Mkabuli ya Kolla Mkoani hapa.
Ikumbukwe Mwaka jana Mtandao huu ulitinga nyumbani kwa hayati Spear Mtaa wa Kigurunyembe Mzambarauni Kata ya Kilakala Manispaa ya Morogoro na kufanya naye mahojiano Maalumu kuhusiana na mafanikio ya kisoka ya Mtoto wake.
Akihojiwa na Mtandao huu jana kuhusiana na kifo cha mpendwa baba yake Abdulrazak alisema.
” Shekidele kama unavyofahamu Mzee wangu aliungua kwa muda mrefu hata kabla mama yangu hajafariki.
Hivi karibuni hali yake ilikuwa mbaya tukaamua kumchukua na kumpeleka Dar kwa matibabu zaidi na jana amefariki dunia muda huu kama unavyotuona ndio tunaingia na mwili wa marehemu kutoka Dar”amesema beki huyo wa Simba ambaye kwa sasa yuko nje ya uwanja akiendelea na matibabu baada ya kumia wakati akiitumikia timu yake hiyo.
Baada ya mahojiano hayo Mwandishi wa Mtandao huu alimfariji Abdulrazack ambaye miaka ya hivi karibuni Mama yake Mzazi Bi Faudhia Ramadhan Mdeng’o naye alifariki dunia wakati yeye akiwa nchini Afrika Kusini akicheza soka la Kulipwa hata hivyo aliwahi kumzika mpendwa Mama yake.
Ama kwa hakika Mzee Mahita kuna swawabu atazipata kwa Mwenyezi Mungu hii ni kwa sababu licha ya kusumbuliwa na Miguu kiasi cha kutembelea vimbo, bado hali hiyo hamzuii kushiriki mazishi ya ndugu na jamaa zake.
Kwenye hili Mwandishi wa habari hizi ni shuhuda kwani amemshuhudia kwenye misiba mingi akiwa sambamba na swahiba wake mKubwa Shehe Koba ambaye ni himamu wa Msikiti wa Mahita uliopo Kata ya Mafiga.

No comments:
Post a Comment