Hilo ni moja ya basi lake la kisasa ambalo lilikuwa likifanya safari zake Dar es salaam kuelekea Nairobi Kenya
Mwandishi wa habari hizi [kati] akizungumza jana na Mhe Malingo pichani[kulia] anayesikiliza mahojiano hayo kushoto ni Mhe Abdallah Ally Meya, aliyekuwa diwani wa kata ya Chamwino ambaye uchaguzi uliopita kwenye kura za maoni ndani ya chama chake cha CCM Kura hazikutosha.
umati mkubwa uliojitokeza makaburi ya Kolla kumzika Mzee HoodNa Dunstan Shekidele,Morogoro.
Mmiliki wa Kampuni ya Mabasi ya Hood, Mzee Mohamed Hood Said amefariki dunia juzi na kuzikwa jana Makabuli ya Kolla mkoani hapa.
Mzee Hood ambaye pia alipata kuwa diwani wa Kata ya Mji Mkuu kwa leseni ya CCM Mwaka 2OOO Mpaka 2005 amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90 huku umati mkubwa wa watu wakijitokeza kumsindikiza kwenye safari yake hiyo ya mwisho hapa duniani.
Kutokana na umaarufu wa Mzee huyo ambaye ndiye Muasisi wa kutoa mabasi ya kuzikia kwa wananchi wa jimbo la Morogoro,mara baada ya kifo chake watu wengi walimlilia kwa kumposti mitandaoni kila mmoja akizungumza mema yake.
Kama kawaida inapotokea tukio kubwa mkoani Morogoro Mtandao huu uja kivingine kuripoti tukio husika, kwa tukio hili la kifo cha Mzee wetu Mwandishi wa habari hizi aliamua kumtafuta diwani wa Kata ya Mji Mkuu aliyeachiwa kijiti na Mzee Hood.
Diwani huyo si Mwingine ni Mhe Hassan Malingo,ambapo baada ya mazishi ya Big Boss huyo wa mabasi ya Hood, Mtandao huu ulizungumza na Mhe Malingo ambaye alikuwa na haya ya kusema.
“ Shekidele kama unavyonijua sikuwa mwanasiasa nilikuwa katibu Mkuu wa timu ya Moro United, nakumbuka mwaka 2004 nikiwa Mwana Mzee Hood alinipigia simu akaniambia hana mpango tena wa kugombea Udiwani kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika 2005 hivyo kwenye uchunguzi wake ndani ya kata yetu ameona mimi naweza kufiti kwenye nafasi hiyo”Alisema Mhe Malingo na kuongeza
“Nikamwambia subiri niongee na Bosi wangu Merey Balhaboo Mmiliki wa timu ya Moro United nikishaongea naye nitarudi kwako”Alisema Malingo.
Je Merey alimkubalia au la stori hii itaendelea kesho hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.





No comments:
Post a Comment