Mjasiliamali Mdogo Stetephen Philipo
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
WANANCHI Wawili mkoani Morogoro,Stephen Philipo na Lamia Abdallah wameamua kutema nyongo kwenye Jumbe walizoweka kwenye vyombo vyao vya usafiri.
Mtandao huu ukiwa kwenye pilika pilika zake za kusaka matukio mitaani ulimshuhudia Limia Abdallah ambaye ni dereva wa boda boda anaye ‘Pack’ boda boda yake Soko la Chief Kingalu akiandika ujumbe unaosomeka hivi ‘Janja la Kutafuta Jinga la Kuhonga’.
Mara baada ya kumpiga picha Mtandao huu ulizungumza naye na mahojiano hayo yalikuwa hivi.
Mwandishi. Habari yako Afisa usafirishaji.
Lamia. Hoo safi Shekidele Mwandishi bora Morogoro nambie.
Mwandishi.Poa, kwa nini umeandika ujumbe huu umemfumbia mtu au una kuhusu wewe mwenye?
Lamia. Unanihusu mimi mwenyewe, ni kweli nambambani sana kutafuta pesa lakini mwisho wa siku matumizi ya hizo pesa ni kuhonga.
Mwandishi. Una mke?
Lamia. Ndio.
Mwandishi.Kwa nini sasa unakuwa Jinga la kuhonga ili hali una mke?
Lamia. Haa Shekidele hizo pesa za matumizi ninazo mpa mke wangu sindio na honga,maana ya ujumbe huu ni kwamba napambana kutafuta pesa kwa lengo kuu la kutunza familia yangu na si vinginevyo.
Mwandishi. Kutunza familia sio kuhonga nio kuhudumia kuhonga mara nyingi imezoeleka kumpa pesa hawara a.k.a mchepuko.
Lamia. shekidele kumpa pesa Mwanake yoyote awe mke wako au sio mke wako ni kuhonga tu hujaona mtu anamuhudumia mkewe wake mwisho wa siku huyo mwanamke anamkimbia sasa anakwenda kwa mwanaume mwingine ,kuhudumia ni kwa mzazi wako ambaye hawezi kukukimbia hata kama ukifirisika.
Mwandishi, Du haya bhna ila binafsi sikubaliani na hoja zako hizo.
Lamia. Sawa Shekidele unauhuru wa kukubari au kutokubali lakini yangu ndio hayo.
Siku iliyofuata Mtandao huu ulikutana na
Steven Philipo Soko la Mji Mpya ambaye mbele ya baiskeli yake aliweka bango lenye ujumbe unaosomeka hivi ‘Shida ingekuwa Sumu tungekufa wengi’ nikamuliza kwa nini umeandika hivyo majibu yake haya hapa.
“ Namshangaa sana Mungu yaani Broo mimi ninashida nyingi sana lakini nashangaa sifi, kama shida zinaua basi tungekufa wengi”alisema Philipo na kuongeza.
“Kwa ukumbwa na jambo hilo licha ya shida zangu niliamua kwenda Stationary nikatoa buku langu kuandika ujumbe huu kueleza ulimwengu”alimalizia kusema jamaa huyo ambaye anafanya biashara ya kuua Matango na Mihogo ya kutafuna.




No comments:
Post a Comment