Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, January 9, 2026

VITUKO VYA MWEZI JANUARI


 

Mwezi uliopita tumeshehelekea Siku Kuu mbili X Mas na Mwaka Mpya.

 

Mwezi huu dume January tunashehelekea kulipa Ada za Shule na kodi za nyumba.

 

Vile vile kuna wengine mwaka mzima wanahifadhi fedha na Mazao yao januari ikifika wanatumia pesa na Mazao hayo kuwacheza Ngoma watoto wao.

 

Utastaajabu Januari hiyo hiyo ikifika wakati wa  kuwalipia ada watoto wao watu hao hao wanalalamika maisha magumu mwezi huu wa Januari, nahisi baadhi ya watu ugumu wa maisha wanautengeneza wenyewe.

 

Pichani Mwandishi wa habari hizi akiwa na Mwanafunzi’Dent’ Neema Dunstan Shekidele.

PONGEZI KWA MHE MAKONDA.MTANDAO

  Mtandao huu unampongeza Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe Poul Christian Makonda kuteuliwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan Kuwa Waziri wa Hahari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.

 

Ikumbukwe kabla ya Utezi huo uliofanya jana Alhamis Januari 8 Mhe Makonda alikuwa Naibu waziri wa wa Wizara hiyo,ambapo akiwa naibu waziri aliingoza timu ya Taifa ya Tanzania nchini Morocco kufudhu kwa Mara ya kwanza hatua ya 16 ya michuano ya Mataifa ya Afrika ‘AFCON 25’.

Pichani Mwandishi wa habari hizi [kushoto]akizungumza na Mhe Makonda.


 

VITUKO VYA MWEZI JANUARI

  Mwezi uliopita tumeshehelekea Siku Kuu mbili X Mas na Mwaka Mpya.   Mwezi huu dume January tunashehelekea kulipa Ada za Shule na kod...