Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, December 18, 2024

UCHAGUZI SERIKALI YA MTAA MJUMBE AWALALAMIKIA WENYEVITI WA MITAA.


  Mjumbe Sanga akizungumza na Mtandao huu.


Na Dustan Shekidele, Morogoro.

MWENDELEZO wa Stori kali ya wiki, ndani ya Mtandao pendwa wa shekidele, Mjumbe wa serikali ya Mtaa wa Lukobe Juu  Jastini Sanga Sammy ametema ‘nyonga’ akiwalalamikia baadhi ya wenyeviti wa Mitaa kutembea na Muhuri wa ofisi  mifukoni mwao.

 Mjumbe huyo kwa leseni ya CCM alitoa malalamiko hayo juzi alipofanya mahojiano maalumu na Mwandishi wa habari hizi aliyetia timu, kuzungumza na Mwenyekiti Joseph  Kamanga  Mwenyekiti pekee wa upinzani aliyeibuka mshindi kwenye uchaguzi wa serikali za Mtaa uliofanyika mwezi uliopita.

Kwenye uchaguzi huo CCM walishinda mitaa 293 na Chadema kupitia kwa Kamanga wakishinda mtaa mmoja wa Lukobe Juu huku wajumbe wake 5 wote wakitoka CCM.

lli kutoa uhuru wa kujieleza kwa maana ya kusema mazuri na mabaya ya mwenzake Mwanahabari huyo aliamua kufanya mahojia chemba na viongozi hao,akianza na mwenyekiti ambaye maelezo yake yaliruka jana kwenye mtandao huu.

Baadae Mwanahabari huyo akamtoa nje Mwenyekiti na kumwingiza ndani Mjumbe Sanga,ambaye alipoulizwa kwa siku 19 yeye na wajumbe wenzake  wanafanyaje kazi na Mwenyekiti kutoka Chama Kingine?.

Mjumbe Sanga alijibu.

” Niwe mkweli mpaka sasa tunafanya kazi vizuri labda huko mbele kuwe na mabadiliko kama ulivyosema hata mwezi bado toka tuanze kazi sijaona baya lake.

Ila kuna kasoro moja Muhuri wa ofisi Mwenyekiti anatembea nao mfukoni anaweza kukuachia ofisi lakini muhiri hakuachii,anakuja mwananchi anahitaji hudumu ya Muhuri, kama yuko jirani unampigia simu anakuja na kama yuko mbali basi Mwananchi inamradhimu akodi boda boda afuate hudumu ya muhuri huko aliko”alisema mjumbe huyo na kuongeza.

Nalisema hili si kwa sababu bosi wangu anatoka Chadema hapapna, tatizo hili ni kwa nchni nzima wakiwemo baadhi ya wenyeviti kutoka chama changu cha CCM.

 Kwa upande mmoja wako sahihi kufanya hivyo kwa sababu muhuri  umeandikwa mwenyekiti  wa Mtaa na sio ofisi ya Mtaa shida iko hapo”alisema Sanga  .

Mwandishi. Ushauri wako ni upi sasa kwa mamlaka zilizotoa Muhuri huo.

Mjumbe Sanga. Ushauri wangu ule Muhuri uandikwe ofisi ya Mtaa sio Mwenyekiti wa Mtaa, ili kama hivi mwenyekiti akinikabidhi Ofisi anikabidhi na huo Muhiri, mfano mtu anakukabidhi gari halafu funguka kaondoka nayo unaliendesha je?

 Kufuatia manung’uniko hayo Mwandishi wa habari hizi aliamua kuludi tena kwa Mwenyekiti Kamanga kumuliza kwa nini anatembea na Muhuri mfukoni?

Sikia  majibu yake” Kazi ya Mjumbe sio kusaini mikataba ya wananchi,kazi ya Mjumbe ni kutumwa na bosi wake na kushiriki kwenye vikao vya maaamuzi au vya  migogoro.

Ni kweli muhuri natembea nao kwa sababu nilivyoapishwa  nilikabidhiwa mimi hakukabidhiwa mjumbe, sasa kama nitauacha ofisini umetumika vibaya wakulizwa ni mimi niliyekabidhiwa  nitaendelea kuwachia  ofisi Muhuri naondoko nao”alimaliza kusema Mwenyekiti huyo ambaye mtaa wake uko Lukobe Mjini mwisho wa daladala eneo lenye maduka makubwa. 

Baada ya kukamilisha mahojiano hayo Mwandishi wa habari hizi alimtwangia simu Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Bw Fikiri Juma kwa lengo la kumpongeza kwa ushindi huo mkubwa.

”Asante sana kwa pongezi ni kweli kwenye mitaa 294 ndani ya Wilaya yetu tumenyakua mitaa 293 huku wapinzania wakiambulia mtaa mmoja.

Niko barabarani shekidele kesho saa 4 asubuhi njoo ofisini tuzungumze zaidi”alisema Big Boss huyo wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini. 

No comments:

Post a Comment

MAJAJI 2 WAHUDHURIA IBADA YA KUMUOMBEA KIGOGO WA SUA MAREHEMU DKT MBILU.

         Mchungaji Dkt Rhoda Chamshama akiongoza ibada hiyo Katibu Mkuu wa  KKKT Usharika wa Mji Mpya Mshana akimuaga Mzee wake wa kanisa S...