Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, September 10, 2024

BINGWA WA DISKO AFRIKA MASHARIKI NA KATI AKIFANYA YAKE MOROGORO




KUMBUKIZI

BINGWA wa kusakati Disko Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Maneno  Mohamed Ngedere Maarufu ‘Super Ngedere’ akifanya yake ndani ya Ukumbi wa King Tom barabara ya Stesheni Mkoni Morogoro akishushiwa Sebene na Band ya Maisha Mapya ’Wana Full Vipaji’.

Ifahamike Super Ngedere  alitwaa ubingwa huo Miaka ya 90 akiushikilia  mpaka sasa baada ya mashindano hayo kusimama kwa muda mrefu.

Kabla ya kutwaa ubingwa huo  Super Ngedere awari alitwaa ubingwa wa Disko Mkoa wa Morogoro na baadae ubingwa wa Disko Tanzania uliompa tiketi ya kushirki mashindano hayo makubwa ya Afrika Mashariki na kati.

Kwenye mchezo wa fainali ya kugombea ubingwa huo Super Ngedere akimgaragaza bingwa wa kusakati Disko nchini Kenya Kanda Kid aliyeambulia nafasi ya pili.

Ikumbukwe Super Ngedere Mkazi wa Mji Mpya Morogoro ni kaka wa damu wa Asha Mohamed Ngedere aliyekuwa akiigizwa na kundi la Vichekesho la Original Komedy la Kina Joti, Mpoki, Masanja Mkandamizaji, Wakuvanga na wengineo

 Picha na Dunstan Shekidele Morogoro.


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...