Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, February 2, 2024

RIPOTI MAARUMU MAFURI MOROGORO

Huu sio mto ni maji ya mto kikundi yameshindwa kupenye kwenye daraja na kuingia barabara ya Makongoro.
Hapo sasa lundo la Magongo likiwa eneo la daraja la Madaraka baada ya magogo hayo kushindwa kupenye kwenye daraja hilo
Moja ya maduka ya simu yaliyopo barabara ya Korogwe,katikati ya Mji wa Morogoro

.....Muonekana wa barabara ya Korogwe baada ya maji kukauka
           ....Tingatinga likizoa tope barabra ya Makongoro
....Muonekano wa barabra ya Makongoro baada ya maji kutoweka
Tatizo liko hapa licha ya daraja la barabara ya Makongoro kuwa fupichini limeweka tutu ambalo kiuhalisia linachangia kikiasi kikubwa mafuriko hayo


.....Lundo la maji likiwa eneo la barabara ya Makongoro
....Wananchi waliotinga katikati ya mjini kununua mahitaji mbali mbali wakishuhudia lundo la Maji barabara ya Makongoro






 


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Takribani Siku 3 Mwandishi wa Makalla hii Dunstan Shekidele’Ez Come Ez Go’alikuwa jijini Arusha kwenye Kazi Maalumu, baada ya kurejea  Mkoani Morogoro alikutana na ishu ya Mafuriko

yaliyosababishwa na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.

Vyombo vingi vya bahari Mkoani Morogoro ikiwemo Mitandao ya Kijamii kwa pamoja wameripoti vizuri  janga hilo la Mafuriko.

Kila ukiwasha Data unakutana na Clip Video za Mafuriko ya Morogoro, ukisoma Magazeti na kuangalia Tv unakutana na Stori za Mafuriko ya Morogoro kila Mwandishi akitoka na ‘Engo’ yake nzuri.

Kwa upande wa Mwandishi wa Mtandao huu yeye ana kwenda mbali zaidi ya stori hizo  akitoka na ‘Engo’ ya Ripoti Maalumu ya uchunguzi wa Mafuriko hayo yanayotokea mara kwa mara maeneo mbali mbali ya Mji wa Morogoro. 

Ripoti hiyo inaonyesha Maeneo yaliyoadhirika zaidi ni Mtaa wa Mazimbu Road eneo la kwa Bwana Jella na Mitaa mitatu yiliyopo katikati ya Mji,Mitaa hiyo ni Madaraka wa Madaraka, Mtaa wa Makongoro na Mtaa wa Korogwe.

lfahamike mitaa hiyo Mitatu inaMaghorofa mengi yenye maduka Makubwa na Taasisi za Kifedha ‘Mabank na soko kuu la Manispaa ya Morogoro Maarufu soko la Kingalu.Uchunguzi wa kina uliofanywa na Mwandishi wa Makalla hii umebani chanzo kikubwa cha mafuriko ya Mitaa hiyo mitatu ya katikati ya Mji kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na Mto Kikundi uliokatiza katikati ya Mji.

Ripoti hiyo imebaini madaraja matatu ya mto huo yaliyopo barabara ya Madaraka, barabara ya Makongoro na barabara ya Korogwe ni mafupi mno huku daraja la Makongoro likiwa na tuta chini hali hiyo inasababisha magogo makubwa yanayosombwa na maji hayo kutoka juu ya Milima ya uluguru kushindwa kupenya kwenye madaraja hayo.

Hali hiyo inapelekea madaraja hayo kuzibwa na magogo hayo na maji kujaa na kutapita kwenye barabara hizo tatu na mwisho wa siku maji hayo yanajaa kwenye maduka na Mabank.

Baadhi ya maduka hayo yanauza bidhaa mbali mbali zikiwemo simu,  Tv,Radio,Umeme wa Sola ambapo bidhaa   zote hizo ni adui  mkubwa wa Maji.

 Baada ya mafuriko hayo kuingia kwenye maduka hayo bila hodi bidhaa hizo ambazo maji ni kirusi kikali, ziliogerea na kupiga mbizi  kama kambare.

Kuona hivyo wamiliki wa maduka hayo wengi wao wakiwa Wachaga’Mabwashee’ na Watanzania wenye asiri ya lndia’Wahindi’ kwa pamoja walikusanya mikono yao yote miwili wakajitwisha kichwani huku wakishuhudia kundi la maji likizama kwenye maduka yao huku Mvua akiendelea kunyesha kwa zaidi ya masaa 2 mfurulizo.

Mvua ilipokata baada ya muda Maji yalikauka likabaki tope zito kwenye barabara hizo za viwango vya Lami lakini kutokana na tope hilo zinaonekana kama barabara za vumbi. Mwandishi wa makalla hii alishuhudia tingatika likisomba tope hizo na kuzipakia kwenye malori ya halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na kwenda kuzitupa dampo.

                                USHAURI.

Mwandishi wa Mkalla hii anaushauri uongozi wa Mkoa wa Morogoro kama kuna uwezeka kuahamisha mto huo usikatize katikatika ya Mji, Peni nia na dhamira hakuna lisilowezekana, Mto huo mdogo unaweza kuchepu,liwa huko huko juu ya Milima ya na kuunganishwa na Mto Mkubwa wa Morogoro ambao pia unatoka huko huko juu ya Milima.

 Mto  kikundi  baada ya kukatiza katikati ya Mji uklfika eneo la Nunge daraja la Reli unaungana na Mto Morogoro  kuelekea  baharini jijini Dar es salaam ukiungana na Mto Ruvu wa Mkoani Pwani.

 Ikishindikana kuhamisha mto huo basi madaraja hayo matatu yatanuliwe kutoa nafasi ya magogo kutoka juu ya Milima kupira kwa urahisi maeneo hayo.

MAFURIKO ENEO LA MAZIMBI ROAD.

Eneo la Mazimbu Road kwa bwana Jella miaka ya nyuma hatukuwahi kusikia ishu hizo za mafuriko, hivyo ripoti kamili inaendelea na uchunguzi kubaini hali hiyo inasababishwa na nini kwa hivi sasa?

Baada ya mafuriko kuzingira eneo hilo la Mazimbi Road imewaradhimi waokoaji wa Jeshi la wananchi wa Tanzania [JWTZ] kutinga eneo hilo na Vifaa maalumu ya uokoaji na kufanya kazi ya kuwavusha watu kutoka eneo moja kwenda eneo linguine.

Endelewa kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...