Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, January 28, 2024

UTALII WA NDANI.



 


Mwandishi wa Mtandao huu akiwa mitaa ya jiji la Arusha eneo la Kaloleni alipotembelea Jumba la Makumbusho ya Azimio la Arusha na kujionea vitu mbali mbali kwenye Jumba hilo lenye histori kubwa ya nchini yetu ya Tanzania.

Saturday, January 27, 2024

KIJIWE NONGWA. UKIONA KAFUTA BANGO UJUMBE UMEFIKA











 


Na Mpekunyuzi wa Mitandao Dunstan Shekidele.

Kama kawaida mtumishi wako, kila wiki naweka Bando linalonitembeza kwenye Mitandao ya Kijamii kukusanya jumbe mbali mbali.

Miongoni mwa jumbe hizo ni za Kuelimisha, Kukosoa na Maneno ya hekima yanayotukumbusha kuwa jirani na Mwenyezi MUNGU.

Tukutane Wiki Ijayo kwa mabango Mengine yenye Jumbe Moto Moto.

Friday, January 26, 2024

MICHUANO YA NDONDO CUP YASHIKA KASI MORO.


Kipa wa Obama Fc akifoka huku akipanga Ukuta wake baada ya Black People kupta Faulo nje ya 18 .




Foka foka ya kipa huyo imesaidi kuudaka mpira huo, kufuatia uimara wa ukuta huo uliojengwa na mabeki wake wakiongozwa na Richard Maarufu Richi' Kulia ambaye anakipiga kwenye moja ya timu za ligi kuu ya Visiwani Zanzibar.
...Hii sasa Papatu Papatu ya Kipa wa Obama Fc na Mshambuliaji wa Black People Fc




...Hwani na Mashabiki wa timu ya Obama Fc wakishangilia ti,mu yao kabla mpira kuanza mwisho wa siku timu yao ilicheza kichapo cha chuma 1-0

 

Na Dustan Shekidele,Morogoro. 
 
MICHUANO ya Ndondo Cup’Super Eight 2024’ inazidi kushika Kasi uwanja wa Saba saba Mkoani hapa. 
 
Miamba Nane kutoka kata mbali mbali za Manispaa ya Morogoro zinapambana kwenye michuano hiyo kuwania kitita cha Milion 3 ‘Cash Maney’.
 
Mkwanja huo umewekwa mezani na Mdhamini wa Michuano hiyo iliyoanza kutimua vumbi January 22 kwa mchezo wa mtani jembe kati ya Black People na wenyeji wa michuano hiyo Obama Fc.
 
Gemu hiyo iliyojaa fundi kwa muda wote wa dakika 90 kufuatia mastaa wengi wa Ligi kuu kuzitumikia timu hizo,Black People’Taifa la Watu weusi kutoka Kata ya Mji Mpya eneo la Kaloleni‘Jijiga’ kwa wajanja iliwatoa nishani wenyeji hao wa Mashindani hayo Obam Fc Kutoka Kata ya Kiwanja Cha Ndege eneo la Mawezi kwa kuwachapa bao 1-0. 
 
Timu Nane zinazoshiriki michuano hiyo ni pamoja na
Moro Talent’kutoka Kata ya Lukobe.
Manzese United Kutoka Kata ya Mafiga.
Black Viba kutoka Kata ya Mbuyuni.
Black People Kutoka Kata ya Mji Mpya.
Bajaj Fc kutoka Kata ya Mbuyuni eneo la SUA.
Washashi Fc Kutoka Kata ya Mji Mpya.
Obama Fc Kutoka Kata ya Kiwanja Cha Ndege.
Na Damu Chafu Fc Kutoka Kata ya Mwembesongo eneo la Mafisa jirani kabisa na nyumbani kwa mchezaji anayecheza soka la kulipwa Ulaya Kelvin John’Mbambe wa Mji Kasoro Bahari.
Katika michuano hiyo mshindi wa kwanza akajinyakulia Milion 2 huku mshindi wa Pili akiondoka na Milioni Moja.
Michuano hiyo inaendeshwa kwa mfumo wa mtoani’Ngumi Jiwe’ ukifungwa unaaga mashindano. 
 
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa January 23 Washashi Fc Wajanja kutoka Mji Mpya kwa Kapetela waliinyuka timu ngumu wa Black Viba kwa Pelnaty 3-2 baada ya dakika 90 timu hizo kutoka sale ya bao 1-1. 
 
Juzi January 24 Vijana wa Kelvin John timu ya Damu Chafu Fc waliwaodnoka mashindanoni Matajiri Bajaj Fc inayomilikiwa na madereba wa Bajaj kwa kuichapa bao 3-1 na kuwatupa nje ya mshindano hayo wakiwapa tiketi ya kwenda kubeba abiri wao wa SUA Mjini, Kasanga. Mjini. Mindu’Mjini. Kihonda’Mjini. Bingwa Mjini. Tubuyu-Mjini. Nane Nane Mjini. Manyuki Mjini., Lukobe Mjini. Mkundi-Mjini.

Tuesday, January 23, 2024

RAS WA KUKU WA NDOO ANDAA MICHUANO YA NDONDO CUP.






 


MKALI wa kuza kuku wa ndoa Mkoani Morogoro Mohamed Chuli. Maarufu Rasta Msafi, amendaa michuano ya Ndondo Cup.
 
Akihojiwa jana na Mwandishi wa habari hizi kwenye uzinduzi wa michuano hiyo inayofanyika Uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro, Babu Chuli amefunguka mazito habari na picha kali za michuano hiyo zitaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...