Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, September 8, 2023

KUMBUKIZI HII NI MWAKA 2017.

Meneja wa tigo kushoto akimkabidhi zawadi ya simu Dustan Shekidele

 


             Na Mwandishi wetu Morogoro.

Mwandishi wa habari wa Mtandao huu,Dustan Shekidele’Mkude Simba’ ameibuka kidedea katika shindano la Jaza Ujazwe la Mtandao wa simu waTigo na kukabidhiwa zawadi.

 

Makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na Meneja wa tigo mkoa wa Morogoro yamefanyika katika ofisi za tigo mkoa  zilizopo katikati ya mji jirani na stendi ya zamani ya daladala.

 

Akizungumza baada ya kumkabidhi simu hiyo Meneja huyo Rashid Abdullahaman alisema Shekidele aliibuka mshindi katika shindano hilo baada ya kuweka vocha na kujiunga katika vifurushi mbali mbali

 

.” Shindano la Jaza ujazwe kinafanyika kila mwezi na mwezi wa 8 Shekidele ameibuka mshindi  tunajisikia fahari kwa Mwandishi wa habari Maarufu nchini kujishindia simu Janja ya Tecno S1 MB na muda wa maongezi kwa mwaka mzima, na toa wito kwa wananchi wengine kuendele kutumia Line za tigo na kuweka vocha mara kwa mara, mbali ya simu zawadi nyingine zinazotolewa katika shindano hilo ni Pikipiki”alisema Meneja huyo.

 

Kwa upande wake Shekidele baada ya kukabidhiwa zawadi hizo afunguka hivi.

 

“ Waandishi wa habari mlivyo jaa mbele yangu na kamera yenu nimejiona kama nimevaa viatu vya Mheshimiwa Rais,  mnasubiri kwa hamu mtumbue mtu badae nikajistukia kumbe ni mimi mkude Simba  Dustan Shekidele’Mtoto wa Mkulima’ kutoka Lushoto  Milima ya Usambara.

 

“ Baada ya maneno hayo ya utani  nijeree kwenye mazungumzo yangu ya msingi, kwamba zaidi ya miaka 6 natumia mtandao wa tigo unaotumiwa na watu wote, wenye maisha ya kawaida maisha ya kati na maisha ya juu.

Nakumbuka juzikati nilipigiwa simu na dada mmoja aliyejitambulisha kwamba yuko tigo makao makuu jijini Dar kanipa hongeza akidai nimeshinda shindano la Jaza ujazwe.

 

” Nikamwambia mbona sijawahi kucheza bahati nasibu akaniambia ninapoweka vocha moja kwa moja naingia kwenye shindano hilo baada ya  maelezo hayo kanimbia Septemba 6 -2017 saa 4 asubuhi nifike ofisi za tigo Morogoro nikabidhiwe zawadi hizo nilizolabidhiwa Meneja pamoja na Afisa mwingine wa kike.aliyenikabidhi nyaraka za simu hiyo

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...