Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, January 15, 2023

UJUMBE WA NENO LA MUNGU   MAFUNDISHO JUU YA TALAKA.


 

 

MARKO 10.2 -12

“Basi Mafarisayo Wakamwendea Wakamwuliza.Je ni halali mtu kumwacha Mkewe?Huku wakimjaribu.

 

Naye akajibu,akamwambia Musa aliwaamuru nini.?

 

Wakasema Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha.

 

Yesu akawaambia kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hiyo.

 

Lakini tangu Mwanzo wa kuumbwa Ulimwengu aliwafanya Mume na Mke.

 

Kwa sababu hiyo Mtu atamwacha,babaye na Mamaye ataambatana na mkewe.

 

Na hao wawili watakuwa mwili mmoja hata wamekuwa si wawili tena bali Mwili Mmoja.

 

 Basi alichounganisha Mungu Mwanadamu asikitenganishe.

 

Hata nyumbani  tena wanafunzi wakamwuliza habari ya neno hilo.

 

Akawaambia kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa Mwingine azini juu yake.

 

Na Mke akimwacha mumewe na kuolewa na Mtu Mwingine azini”. Hilo ndilo neno letu la leo Jumapili ya January 15.

 

    UCHAMBUZI WA NENO HILO.

Kwa ujumbe huo inaonyesha  Mungu na mitume wake wote nachukizwa sana na watu kuachana, katika hali hiyo Mafarisayo walimtega yesu wakimuliza swali hilo la watu kuachana.

 

Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya usariti kwenye ndoa hamna namna Musa aliamua kutunga sheria ya watu kupeana talaka kunusuru majanga zaidi kwenye familia.

 

Yesu naye kubariki hilo kwa shingo upande akisema kweli Musa alitunga amri hiyo ya kuachana kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu.

 

Ugumu huo uko wa aina nyingi ikiwemo tamaa za Mali na tamaa za ngono mtu anamke  au mume  anakwenda kuzaa nje ya ndoa kiuhalisi huyo mwenzi wake atakubaliana na hali hiyo.

 

 Kwenye Bibli hiyo hiyo kuna mahali nilisoma wanafunzi wa Yesu walimuliza swali wakisema’ Mwalimu kama ndoa za kikristo hazivunjiki mpaka mmoja atakapo kufa je nikimfumania mke wangu itakuwaje.?

 

Yesu akawajibu ndoa hiyo hiyo itavunjika kwa uzini lakini uwe uzini wa kuthibitisha usio na shaka yoyote sio umemkuta mkeo kakaa baa na Mwanaume wana kunywa unasema umemfumani ndoa ivunjike hapana.

 

 Kwenye eneo hilo Yesu ameweka wazi kwamba yule anayevunja ndoa kwa sababu tu amepata Bwana mwenye pesa au Mwanaume amepata Mwanamke mrembo hao wakifunga ndoa wanajidanganya wanazini tu hakuna ndoa hapo.

 

 

Aliyeachwa anakuwa salama kwa sababu si yeye aliyevunja ndoa, kwenye kiapo cha ndoa  aliyepewa kibari cha kufungisha  anamalizia kwa kusema.

 

“Alichokiunganisha Mungu Mwanadam awaye yote asikitenganishe ndoa hii iheshimiwe na watu wote”.

 

 Kwenye kiapo hicho wazazi na wanandoa wenyewe  wameaswa na Mungu  asitokee mtu yoyote kuvunja ndoa hiyo.

 

 Hivyo wenzangu na Mimi tulioachwa tusihuzunike sana tuendelee kumtumaini Mungu kwenye magumu tunayopitia kuna maisha mengine baada ya kuachwa.

 

Nahisi kwenye eneo hili Mungu atawasamehe wote walioachwa kwamfano mtu anampenda mke au mume hayuko tayari ndoa yao ivunjike lakini mmoja wao  anamfanyia visa Mwenzi wake.

Kwa sababu anampenda na hayupo tayari ndoa yao ivunjike anamua kujishusha na kuomba msamaha kwa lengo la kulinda ndoa yake. Lakini mwenye dhamira ya kuvunja ndoa hiyo anaendelea kufoka huku akishinikiza kutoa talaka.

 

Masikini ya Mungu  mwisho wa siku anakupa talaka wakati wewe hujajipanga kuvunja ndoa yako lakini kwa sababu muhusika kashikilia msimamo wake basi huja jinsi inabidi ukubariane na hali halisi.

 

 Wakati ukikonda kwa msongo wa mawazo  ya kuachwa baada ya muda mfupi unasikia Mumeo au mkeo anaishi na mtu mwingine inauma sana.

 

Nawahisi wanadamu wenzangu  tusifanya hivyo ni chukizo kubwa mbele za Mungu naamini hata huyu uliyempata kwa dhambi hii kubwa hamuwezi kukaa salama.

 

Hao waliovunja ndoa kwa sababu za tamaa za Mali, Mwili na Pesa tuwaache wapingane na sheria za Mungu tutaonana kesho kwenye hukumu ya milele.

 

Na tulio kwenye ndoa zaidi ya miaka 3 na kuendelea nawa pongezi nyingi tunajua kwenye ndoa sio peponi kwamba kila siku ni raha hapana kuna nyakati za furaha na nyakati za maumivu hivyo nawasihi na tuvumiliane kwenye nyakati zote ikitokea tumekwaluzana  basi tuombane msamaha maisha ya ndoa yaendelee kwa utukufu wa Mungu.

 

Tubebeane Misalaba kwenye ndoa zetu kwani hakuna Mwanadamu aliyekamilika wote tunamapungufu Mkamilifu ni Mmoja tu Mungu aliyeumba mbingu na ardhi lakini Mbwa, Ngedere, Paka, samaki na binadamu wote tuna mapungufu.

Hivyo usimuhukumu mkeo au mumeo kwa mapungufu yake ili hali na wewe unamapungufu yako anayavumilia.

 

Kwenye ndoa zetu tuwe kama huu mzani pesa tena dora iko chini Upendo uko juu, kizazi cha wengi wao Pesa iko juu upendo uko chini ndio maana ndoa nyingi hazidumu.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...