Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, November 19, 2022

UWANJA WA CCM SABA SABA UMEEZULIWA MABATI MASHABIKI WAJA JUU,MENEJA AFUNGUKA.





 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
 
UWANJA wa CCM Saba Saba unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi’CCM’ Mkoa wa Morogoro, unaotumika kwa ligi mbali mbali ikiwemo ligi kubwa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania’F.A Cup’Maarufu Azam Sports Federation Cup,umeezuliwa mabati zaidi ya 6.
 
Kufuatia hali hiyo baadhi ya Mashabiki wa Soka Mkoa wa Morogoro wameulalamikia Uongozi wa Uwanja huo kwa kutochukua hatua zozote kukabiliana na uhalibifu huo.
 
” Lilianza kuezuliwa bati moja Uongozi wa Uwanja haukuchukua hatu yoyote kudhibiti hali hiyo mpaka sasa yameezuliwa mabati 6 na bado yanaendelea kuezuliwa kipindi hiki cha mvua inayoambatana na upepo mkali,hakuna hatua yoyote inayochukuliwa kunusuli Uwanja huu ambao ni maarufu sana hapa Morogoro”alisema shabiki aliyejitambulisha kwa jina la Shomari Juma. 
 
Kufuatii malalamiko hayo Mwandishi wa habari hizi alimtafuta kwa njia ya simu Meneja wa Uwanja huo Joseph Fredrick Makalla alipoulizwa alisema.
 
” Nikweli mabati kadhaa yameezuliwa na upepe kwenye uwanja wetu wa Saba saba kwa bahati nzuri mabati yote tumefanikiwa kuyaokota baada ya kupepeluka kinacho kwamisha ni fundi niliyempa kazi ya kuyaludisha tena kwenye paa anaonekna kuwa bize na kazi nyingine tumepatana juzi afanye kazi hiyo lakini hakufanya nikuhakikishie Shekidele ndani ya wiki hii tutaifanya kazi hiyo na uwanja utareja kwenye hali yake ya kawaida”alisema Meneja huyo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi eneo la Bingwa.
 
Baadhi ya wafanyabiasha wa Mnada wa Saba saba walidai kwamba Meneja huyo kila siku anakuja na mafundi wanapisha kwenye utendaji kazi.
 
“Shekidele tatizo sio mafundi tatizo ni Meneja mafundi baada ya kukagua waliona mbao zote za kench zimeoza kwa hiyo wanaogopa kufa kwa kushuka na chini na baa hilo.
 
Pia walisema misumari haingia kwenye bao hizo zilizoliwa na wadudu zinabonyea kama sponnji.
 
Walichoshauli mafunioa ni kwamba baa lote lishuke chini wasuke mbao Mpya kisha waludishie mabati hayo kinachoonekana Uongozi wa Uwanja hawako tayari kufanya hivyo kwa sasa tatizo ndio hilo Shekidele mabati yote yaliyoezuliwa sisi tumeyaokota haya hapa juu”alisema Bavoni Kaloli
 
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro’MRFA’ Emmanuel Kimbawala alipotakiwa kuzungumza hali hiyo alisema
 
” lnasigitisha sana Shekidele hali hii imetokea kipindi hiki cha Mvua ambapo kwenye michuano mbali mbali Wageni mashuhuri tunaowaalika huketi eneo hili pia baadhi ya mashabiki inapokea mvua huja kujibanza kwenye eneo hilo dogo lenye baa la bati sasa sehemu kubwa iko wazi kufuatia mabati kutoweka, kesho Jumamosi[Leo] na kesho kutwaa[Kesho] jumapili mimi kama msimamizi wa kituo cha Morogoro nimeamua kuleta michezo ya FA kwenye uwanja huu wa Saba saba Kesho Jumamosi timu yetu ya Moro Kids itakipiga na Silent Ocean ya Jijini Dar na kesho kutwaa Jumapili timu yetu nyingine ya Mkundi United itakipiga na Nyika Fc kutoka Mkoa wa Pwani”alisema Katibu huyo MRFA.
 
Mbali na mabati hayo kuezuliwa na Upepo awari baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa Vibaka waling’oa Mbaadhi ya majukwaa ya uwanja huo yenye Nondo ndani nakuondoka nayo kama inayoonekna Pichani.



No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...