Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, October 12, 2022

MAVETERANI WA MIKOA YA TANZANIA BARA NA VISIWANI KUMUENZI BABA WA TAIFA MORO.

Hyati Mwalimu Nyerere akifanya mazoezi ya kuendesha baiskeli enzi a uhai wake
Wachezaji nyota wa zamani wa Tanzania kushoto Mzee Sundar Manara 'Computer' Hussein Ngurungu'Daktari wa Mpira na Juma a.k.a Anko J kulia
Mshambuliaji hatari wa Moro Veterani Aziz Abood ambaye pia ni taji namba Moja Mkoa wa Morogoro akituliza mpira kwenye Kifua huku akichungw ana beki wa timu ya Dar Veterani
                      Kikosi Kabambe cha Moro Veterani


 Mchezaji hatari wa Moro Veterani Dunstan Shekidele'Mkusw Simba' akijifua kujianda na Bonanza hilo


           Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

TIMU 18 za Maveterani’ Kutoka Mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar zimethibitisha kushiriki Bonanza la Nyerere Day litakalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili mfurulizo.  

 

Tamasha hilo lenye lengo la kumuenzi Mwasisi wa Taifa la Tanzania ambaye pia ni Rais wa kwanza wa Taifa hilo Hayati Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia Octobar 14 1999 nchini Uingereza litafanyika ljumaa Octobar 14 na kufika tamati Jumamosi Octobar 15.

 

Bonanza hilo lililoandaliwa na  timu Kabambe ya Morogoro Veterani litafanyika kwenye Viwanja 4 ambapo timu hizo 18 zimegawanywa kwenye Makundi 4 kundi la kwanza litakipiga  Uwanja wa Shujaa, kundi la Pili, Uwanja wa Saba saba, kundi la tatu Uwanja wa SUA na kundi la 4 Uwanja wa Morogoro Sekondari. Akizungumza na Mtandao huu mmoja wa Viongozi wa Moro Veterani Seleman Msumi amezitaja baadhi ya timu zitakazoshiriki Tamasha hilo ambazo ni Kahawa Veterani ya Zazibari, Dodoma Veterani, na Mafinga Veterani ya Njombe.

 

Nyingine ni Korongwe Veterani ya Korongwe Tanga, Kilombero Veterani ya kutoka Kiwanda cha Sukari Kilombero. Kilunywa Veterani ya Dar  Bagamoyo Veterani ya  Pwani na wenyeji Morogoro Veterani.

 

Kwa mujibu wa Msumi mshindi wa kwanza atanyakua seti moja ya Jezi, Mshindi wa Pili atakabidhiwa Mipita 2 na Mshindi wa 3 atapewa Mpira Mmoja.

 

Kwa mujibu wa waandaji mara baada ya Bonanza  hilo kutamatika siku hiyo ya Jumamosi usiku washiriki wote  watakwenda kumwagilia Moyo kwenye kiwanja cha wajanja mkoani Morogoro  Ukumbi wa kisasa wa Samaki Sport Maarufu Samaki Samaki watu watakula bata mpaka Jogoo la kwanza litakapo winga alfajiri.

lfahamike Mwandishi wa Mtandao huu pia ni Mchezaji hatari wa timu ya Moro Veterani inayopewa nafasi kubwa kutwaa ubingwa na Bonanza hilo.

                 

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...