Mpiga Dram akilipiga Sebene kwa Viungo vyote
Waimbaji vyota wa bdani hiyo kutoka kulia Joshua Malekela, Yahaya Masauti na Abubakar Pugi wakiimba kwenye show hiyo
Na Mlala Nje Dunstan Shekidele,Morogoro.
BENDI ya Maisha Mapya ‘Wana Full Vipaji’ siku ya Mkesha wa Kuaga Mwaka 2021 na kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2022 walikiwasha vile vile kwenye Ukumbi wa Bwalo la Umwena unaomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa’JKT’.
Kutokana na Ubora wa band ya Maisha Mapya Wajeda hao kwa Mara ya kwanza waliamua kuialika kwenye Mkesha huo kwa lengo la kuwatumbuiza hao pamoja na wateja wa ukumbi huo uliopo jirani na Uwanja wa Jamhuri.
Majira ya saa 7 usiku Mlala nje baada ya kutoka Kanisani kwenye lbada ya kuaga Mwaka na kukaribisha mwaka Mpya alitinga kwenye Ukumbi huo na kushuhudia Umati wawatu ukilisakata Sebene la nguvu kutoka kwa Vijana hao wadogo waliokomaa Vichwa kwa ugumu wa Maisha.
Wadau wakubwa wa band ya Maisha Maife na wenzake ambao ni wakazi wa Mtoni Street Kata ya Mbuyuni walipomuona Mlala nje akiwa bize kuwapiga Picha wasanii wa bandi ya Maisha Mapya wao walipaza sauti wakisema.
Shekidele Mlala nje tupige Picha na sisi ukaturushe kwenye Mtandao wako tuuze sura
”Mlala nje alitii agizo hilo na kuwaphotoa mapicha warembo hao na kurusha kwenye mtandao kama wanavyoonekana wakijipa raha wenyewe.
Baada ya kuwa Photo warembo hao walipaza tena sauti safari hii wakiwaamuru wanazumuziki wa Maisha Mapya kuwapigia Wimbo unaosema ‘Sio kila Mwanamke anayekwenda baa anakwenda kujiuza wengine pochi zao zimejaa mapesa yanayotosha hata kuwapa ofa za bia wanaume.
”Wasanii wa Maisha Mapya wanaowadhamini wateja wao walitii Ombi hilo na kugonga Lisong hilo ambapo kundi la wanawake waliamka kwenye viti vyao na kwenda kucheza huku baadhi yao walionyesha jeri ya Pesa kwakuwa mwagia minoti wasanii wa Masiha Mapya.
”Wakati wimbo huo wa wenye mahudhui ya Mipaso kwa baadhi ya wanaume wanaotongoza hovyo wanawake kwenye mabaa ukiwa hewani Mlala nje aliwashuhudia wanaume wengi wakiwa bize na simu zao wakichati huku wengine wakiwasapoti wanawake hao kwa kucheza goma hilo linalopendwa na wanawake wengi.
Mlala nje aliwashuhudia Wajeda wengi pamoja na Mapolisi wakirisakata Sebene zito lililoshushwa na Vijana hao wa Maisha Mapya.
lfahamike pia Ukumbi huo wa Bwalo uko pia jirani na Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Morogoro, baadhi ya Wajeda na Mapolisi wanaomfahamu Mlala nje walimsogelea na kumtakia kheri ya Mwaka Mpya.
No comments:
Post a Comment