Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, January 1, 2022

WAUMINI KKKT WAAGA MWAKA 2021 NA KUPOKEA MWAKA MPYA 2022 KWA VICHEKO NA VILIO.









Mchungaji Sifii Dunia[kulia] akiangusha maombi ya kujiandaa kuupokea Mwaka Mpya na wasaiudizi wake Mwinhilisti Godfray Nyange[kushoto' na Mwinjilisti Jason Tibaganywa

Mchungaji wa KKKT Usharika wa Mji Mpya Morogoro Mch Sifii Dunia akifanya maombi kwa makundi Maalumu kwenye mkesha wa Mwaka Mpya uliofanyika jana kwenye usharika huo Mama wa Daypsisi ya Morogoro.

 



                         Na Dunstan Shekidele,Morogoro

Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania’KKKT’ Usharika wa Mji Mpya Mkoani hapa, jana usiku wamefanya lbada ya kuuga Mwaka 2021 na Kuupokea Mwaka Mpya wa 2022 kwa Vicheko na Vilio.

lbada hiyo nzuri iliyoongozwa na Mchungaji Kiongozi wa Usharika huo, Mchungaji Sifii Dunia  imeanza saa 2 usiku mwaka 2021 na kukamilika saa 7 usiku mwaka 2022.

Katika lbada hiyo ilihudhuriwa pia na Mwandishi wa Mtandao huu ambaye ni Muumini wa Usharika huo ilitawaliwa na Nyimbo yakiwemo Mapambio, Mahubiri na Maombi kwa Makundi mbali mbali.

Mara baada ya kuingia Mwaka Mpya saa 6 usiku kundi la waumini wa Usharika huo walipokea Mwaka kwa hisia tofauti wengine waliluka luka huku huku wakiangua vicheko na wengine walipiga magoti Madhebahuni mwa bwana wakishusha maombi yaliyoambatana na Vilio.

 

Uchunguzi wa awari uliofanywa na Mwandishi wa habari hizi ulibaini kwamba  waliangua vilio wakiwakumbuka wapendwa wao walioaga dunia mwaka 2021 huku wengine wakiangua vilio wakimshukuru Mungu kwa kuwaponya kwenye maradhi na kuwaokoa kwenye majanga mbali mbali wakiamini  wamevuka mwaka kwa Neema za Mungu Pekee.

Baada ya kupokea mwaka Majira ya saa 6 na nusu Mchungaji Dunia alifanya maombi Maalumu kwa watu wa makundi tofauti tofauti ambapo awari aliwaalika madhebahuni, Wafanyabiashara ambapo aliwaombea  biashara zao zikue, baadaye akawaalika Wafanyakazi.

 

 Mtumishi huyo alimalizia maombi hayo kwa kuwalika Wakulima na wafugaji, Wanafunzi wote kuanzia Chekechea Mpaka Vyuo Vikuu na mwisho alihitimisha lbada hiyo kwa maombi  kwa Wasichana na Wavulana wanaohitaji kufunga ndoa Mwaka 2022.

Kalenda na saa ya camera  baada ya kuingia Mwaka Mpya kwa pamoja viligoma kubadilika   na kuingia Mwaka Mpya kama vinavyoonekana Pichani,  baadhi ya Clip Video za Matukio hayo zitaruka hewani hivi Punde endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...