Baada ya mvua kunyesha juzi na jana Mto Morogoro umejaa na kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya kunyauka kwa kile kilichoelezwa ukame
Watoto wakicheza Mpira katikatika ya Mto Morogoro takribani siku 4 zilizopita baada ya Mto huo kukauka kwa Ukame
Daraja la Kichangani
Usafiri makini wa Mwandishi wa Mtandao huu ukiwa juu ya daraja la Kichangani wakati Mwandishi huyo akiwajibika eneo hilo
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
lnasigitisha sana takribani siku mbili toka Mtandao huu kuripoti habari ya watoto kucheza Mpira katikati ya Mto Morogoro eneo la Mtaa wa River Side Kata ya Mwembesongom jirani na daraja la Kichangani.
Watoto hao zaidi ya 20 walifikia uamuzi wa kujenga uwanja eneo hilo hatarishi kwa kile walichodai ni kukosa maeneo ya wazi ya wao kucheza mpira wa Miguu kwa lengo la kuibua na kuendeleza Vipaji vyao.
Juzi na Jana Mvua kubwa imenyesha Mkoani Morogoro hasa maeneo ya Milima ya Uluguru unapoanzia Mto huo.hali hiyo ilipelekea Mto huo kujaa maji ukirejea katika hali yake ya awari na kusomba Magori ya watoto hao.
Kufuatia hali hiyo jana Mwandishi wa Mtandao huu alitinga eneo hilo kwa lengo kujionea hali halisi baada ya Mvua kunyesha.
Kwa masikitiko Makubwa Mwandishi wa Mtandao huu alipofika eneo hilo Majira ya saa 12 jioni aliwashuhudia watoto wawili Othuman pichani kulia na Johackim wakiwa katika majozi makubwa baada ya kushuhudia uwanja wao wa mazoezi ukisombwa na Maji hali iliyopelekea wao kukosa fursa ya kucheza Mpira.
Baada ya jana usiku Mvua kubwa kunyesha leo asubuhi Mwandishi wa habari hizi alitinga tena eneo hilo na kushuhudia Mto huo ukifurika Maji kiasi hata cha watu kushindwa kuvuka kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine huku Maji hayo yakiwana rangi nyekundu tofauti na jana yalikuwa na rangi nyeupe.
Mtandao huu ulipata fursa ya kuzungumza na watoto hao Othuman pamoja na Johackim ambao walieleze masigitiko yao ya kuondokewa na uwanja wao huku wakirengwa lengwa na Machozi.
Clip Video ya mahojiano hayo itaruka hewani hivi Punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment