Kipa wa Viba Mfaume Gumbo ambaye pia ni Kipa namba Moja wa Mawenzi Market akiramba udogo huku baada ya kushindwa kunyaka Mpira unaoonekana Pichani ukitikisa vyama.
.... Bao hilo la kwanza lilifungwa na ldd Kipangwe no 15 anaye kipiga Namungo Fc ya Lindi
...Nasry Scobber ambaye ni beki kisiki wa Mtibwa B akishika ngozo baada ya bao hilo kutinga wavuni
...Hela heka langoni mwa Mtibwa Sugar
Kipa wa Black Viba Mfaume Gumbo akinyaka Mpira huku akizongwa na mshambiuliaji wa Wakushi Mrisho Said 'Ziko wa Kilosa'
...Beki wa zamani wa Simba Miraj Adam Seleman'TATA'
Mshambuliaji hatari wa Wakushi Fc ldd Kipangwe ambaye pia anakipiga timu ya ligi kuu ya Namungo ya Lindi akizungumza na Mtandao huu mara baada ya gemu hiyo kukamilika jioni ya leo. Baada ya ligi kuu kufika tamani wachezaji wengi wamerejea makwao. na Mkoa wa Morogoro unaongoza kwa kutoa wachezaji wengi wanaochezaji timu mbali mbali za ligi kuu.
Miongo mwa wachezaji hao ni Gerald Mathias Mdemu anayekipiga Polisi Tanzania. Kwa sasa mchezai huyo anayeishi Mtaa wa Juhudi zako Kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro kwa sasa anauguza majeraha baada ya kuvunjika miguu yote 2 kwenye ajari iliyotokea Moshi wakati timu hiyo ya ;Polisi Tanzania ikitokea mazoezi.
Ziko wa Kilosakulia] na ldd Kipangwekati] wakipozi mbele ya kamera za Mtandao huu wakiwa na wachezaji wa Viba
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
VIGOGO vya Michuano ya Ndondo Cup Mkoa wa Morogoro Black Viba kutoka Mtaa wa Vibandani Kata ya Mbuyuni inayoongozwa na diwani Samwel Msuya leo jioni imefungasha vilango vya na kuelekea kwao Vibandani, baada ya kuchapwa bao 3-2 na Wakushi Fc yenye Maskani yake Mitaa ya Misufini na Manzese Kata ya Mafiga.
Kama kawaida timu zote zilishehe wachezaji nyota wakiwemo wa ligi kuu huku Wakushi wakiongozwa na Mshambuliaji hatari wa Namungo ya Ruangwa Lindi ldd Kipangwe, beki wa zamani wa Simba Miraj Adam na mshambuliaji wa zamani wa Maji Maji ya Songea Mrisho Said ‘Ziko wa Kilosa’, huku Viba kama kawaida ikiongozwa na wachezaji wa Mtibwa B wakiongozwa na ldrisa Fikiri Magoso’Mtoto wa Beki wa zamani wa Reli ya Morogoro na Simba Fikiri Magoso na Daud Niyonzima kiungo wa zamani wa Ndanda Fc ya Mtwara.
Katika gemu hiyo mshambuliaji huyo wa Namungo ldd Kipangwe alifunga mabao 2 huku Ziko wa kilosa akifunga bao la 3.
Kwa Matokeao hayo Viba wameaga mshindano huku Wakushi Fc wakitinga Nusu fainali wakiungana na Chadongo na Nughutu kesho ni robo fainali ya mwisho kati ya Salange Fc na Moro Kids
No comments:
Post a Comment