Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, March 28, 2026

SEHEMU YA PILI MLEMAVU MATAMA KUJENGEWA NYUMBA NA MUNGU.









               Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

SEHEMU ya kwanza ya habari hii ya kumbukizi ya Mlemavu Mohamed Mtama kujengewa nyumba na Mungu imeruka juzi kwenye Mtandao Pendwa wa Shekidele,Leo tunaendelea na sehemu ya pili.

Wakati mazungumzo  na Mlemavu huyo ya kuibiwa baiskeli  na Vibaka [Mateja] wakaenda  kuuza vyuma chakavu yakiendelea aliomba kwenda chooni kujisaidia.

Choo kilikuwa umbali wa takribani  mita 20 kutoka kilipo chumba chake na kwamba kipindi hicho kilikuwani kipindi cha Mvua za Masika.

 

Mwandishi alishangaa kuona Matama anasindikizwa na mkewe alipouliza, Matama alisema Choo chao kina changamoto nyingi  hivyo kwa hali yake lazima apate msaada wa mkewe.

Mwanahabari huyo alitoka nje na kushuhudia Matama akitambaa na mikono kabla ya kufika chooni alizama kwenye dimbwi la maji machafu.

Kwenye kimfereji hicho wapangaji wenzie waliweka kidaraja cha mbao kuvuka kuelekea Maliwato[Chooni].

Inauma sana Aisee,Choo hicho nimeezekwa na mabati chakavu hivyo kufuatia mvua kubwa ndani kimejaa tope zito lillochanganyika na kinyesi.

Bi Mau Said Mwenye mapenzi ya kweli kwa  Mume’we  alimfungulia Mlango akatambaa na mikonono akaingia kwenye choo hicho kilichojaa tope lililochanganyika na kinyesi.

Ama kwa hakika hali hiyo iliniumiza  Moyo wa Mwandishi wa habari hizi na kwamba ndani ya muda mfupi alisikia  sauti ya Mungu  ikimuagiza kumnunulia baiskeli na kumjengea nyumba kupitia kazi yake ya Uandishi wa habari.

Mwanahabari huyo alitii sauti hiyo na moja kwa moja akamjulisha  Matama kuhusiana na agizo hilo nililopewa na Mungu.

Kama tunavyojua kila kitu kinakwenda na ushahidi hivyo Mwandishi huyo alimuomba Matama ampige picha  aklwa kwenye mazingira hayo magumu na hatarishi kiafya.

Matama alikubali ombi hilo hivyo Mwanahabari huyo aliacha kazi zote na kufanya kazi hiyo aliyotumwa na Mungu ambapo alianzisha harambee ya kumnunua baiskeri na kumjengea nyumba mpendwa wetu huyo harambee hiyo niliifanya kwenye Mtandao pendwa wa Shekidele na kwenye vyomba mbali mbali vya habari.

Wadau wa Mtandao huu wanakumbuka vizuri harambee hiyo,ambapo wengi wao walichangia ujenzi huo huku  wengine walitupatia Cement na wengine Mabati ambapo vitu hivyo tulivisafirisha kwa usafifi wa baiskeli ya Matama na Pikipiki ya Mwandishi wa habari hizi  kwenda kuvihifadhi kwenye chumba cha Matama.

 Mungu awabariki wote mliochangia  mmeweka alama ambayo mtakufa nayo hata kama ulinunua tofari moja.

Mungu Mkubwa ndani ya Miezi miwili Mwanahabari huyo alipata Pesa  za kununua baiskeri na kiwanja.

Wengi walichangia baada ya kuguswa walipoziona  picha za Matama zilisokwenda sambamba na habari ya kusigitisha.

 Mwenyekiti wa Mtaa wa saadan hayati Hassan Msungi pichani mwenye suti  alichangia Loti moja la Mchanga na kuruhusu tofari 300 za msingi zifyatuliwe nyumbani kwake.

 Baadae zitaruka picha za nyumba hiyo toka msingi mpaka kukamilika hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

 

No comments:

Post a Comment

MAJAJI 2 WAHUDHURIA IBADA YA KUMUOMBEA KIGOGO WA SUA MAREHEMU DKT MBILU.

         Mchungaji Dkt Rhoda Chamshama akiongoza ibada hiyo Katibu Mkuu wa  KKKT Usharika wa Mji Mpya Mshana akimuaga Mzee wake wa kanisa S...