Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, March 22, 2026

MWENYEKITI WA MTAA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI AKIELEKEA NYUMBANI KUFUTURU.


Hayati Msungi aliyesimama mwenye suti enzi za Uhai wake.

 

Msemaji wa Familia Ally Msungi aliyeketi akihojiwa na Mtandao huu.

 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

MWENYEKITI wa zamani wa Mtaa wa Saadan Kata ya Mwembesongo kwa leseni ya Chama cha Wananchi CUF,Hassan Hussein Msungi[46]amefariki dunia baada ya kugongwa na gari akiwa na usafiri wake wa Pikipiki akitoka kwenye shughuri zake za utafutaji akirejea nyumbani  kufuturu.

 

Tukio hilo lililowaumiza watu wengi akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Adamu Kigoma Malima, limetokea Jumanne iliyopita barabara kuu ya Morogoro-Dar es salaam eneo la Nane Nane jirani  na Chuo Kikuu cha Jordan kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro.

 

Mara baada ya kumpunzisha Mpendwa wetu kwenye nyumbani yake ya Milele Makaburi ya Mafisa kwa Dala Kata ya Tungi, Mwandishi wa habari hizi alizungumza na msemaji wa Familia ya Msungi. Ally Hussein Msungi ambapo alipotakiwa kueleza tukio hilo alisema.

 

“ Inauma sana Shekidele kaka yangu akiwa kwenye  Pikipiki yake akitokea Kingolwira kwenye biashara zake majira ya saa 12 jioni akirejea nyumbani kufuturu alipofika Jordan jirani na ukuta wa uwanja wa Maonyesho ya Kilimo[Nane Nane] aligongwa na Gari na dereva huyo amekimbia akimuacha kaka yangu akigaragara kwenye lami zaidi ya dakika 15 bila kupata msaada”Alisema Msemaji huyo wa famia na kuongeza.

 

“Kiukweli dereva huyo ametukosea sana barabarani ajali ni jambo la kawaida angesimama ametuduma ya kwanza kaka yangu,Kama unavyojua giza lilishaanza kuingia na madereva wengi walimkwepa na kuendelea na safari baada ya kupita muda mrefu kuna dereva mmoja msamalia mwema alipofika kituo cha mabasi  Nane Nane aliwaambia boda boda  kwamba pale Jordan kuna boda boda mwenzao amegongwa na anatokwa na damu nyingi.

 

Kundi la Boda boda walifika eneo la tukio na kwa bahati Boda mmoja amemtambua kaka yangu na kutupa taarifa huku wengine wakimkimbiza kituo cha Afya Nane nane kabla ya kuhamishia hospital ya Mkoa wa Morogoro”amesema Msungi na kumalizia kwa kusema

 

“Hali ya kaka iliendelea kuwa mbaya na Mkuu wa Mkoa Mhe Adam Malima alitoa usafiri ili tumkiombize Muhimbili wakati jitihada hizo zikiendelea Mpendwa kaka yangu alifariki dunia akiwa kwenye mikono ya Madaktari waliokuwa wakipambania uhai wake”Alisema Msemaji huyo huku akirengwa rengwa na machozi.

 

Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Saadan kupitia leseni ya CCM Ally  Hussein Msungi aliyemshinda mgombea wa CUF Hassan Husein Msungi,akihojiwa na Mtandao huu kwa kofia yake  ya Uwenyekiti wa Mtaa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

 

Baadae Mtandao huu utarusha Wasifu Mzito wa hayati Msungi ambaye alikuwa  Kiongozi wa CUF Wilaya, alikuwa Mwanaharakati wa Umoja wa Vijana wa Kiislam katika Taasisi ya Tanzania inayojihusisha na kutoa Misaada kwenye Vituo vya Watoto yatima.

 

Aidha Mtandao huu utasimulia Hayati Msungi alivyopambana kwenye uchaguzi wa serikali ya Mtaa na Mdogo wake  hivyo nakusihi endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

                


 

 

 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MAJAJI 2 WAHUDHURIA IBADA YA KUMUOMBEA KIGOGO WA SUA MAREHEMU DKT MBILU.

         Mchungaji Dkt Rhoda Chamshama akiongoza ibada hiyo Katibu Mkuu wa  KKKT Usharika wa Mji Mpya Mshana akimuaga Mzee wake wa kanisa S...