Hayati Hassan Hussein Msungi aliyesimama enzi za Uhai wake.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
FAMILIA ya hayati Mzee Hussein Msungi wanakipaji cha Uongozi?
Jibu la Swali hilo unaweza kulipata kwenye Stori hapo chini.
Toka Mwaka 2009 Mtaa wa Saadan Kata ya Mwembesongo Mkoani hapa unaongozwa na familia ya Msungi.
Hii si kwa bahati mbaya bali ni kipaji cha Uongozi walichojaliwa Familia hiyo ya Msungi.ambapo Mwaka 2009 Hassan Msungi akiwa kijana Mdogo alijitosa kugombea nafasi ya Uwenyekiti wa Mtaa wa Saadan kwa leseni ya Chama Cha Wananchi [CUF] na kufanikiwa kuibuka kidedea baada ya kuwashinda Wagombea wa vyama vingine akiwemo Mgombea wa Chama tawara ‘CCM’
Huku akiongozwa na hofu ya Mungu kufuatia kuisoma Dini ya Kiislamu vizuri,aliwatumikia kwa uaminifu mkubwa Wananchi wake hali iliyopelekea kushinda kwa kushindo kwenye uchaguzi uliofanyika Mwaka 2014.
Kufuatia hali hiyo Uchaguzi wa Mwaka 2019 Uongozi wa CCM Kata ya Mwembesongo “ulijiongeza’na kuamua kumpitisha Ally Msungi kupambana na kaka yake.
Katika uchaguzi huo Mdogo mtu Ally Msungi alifanikiwa kushinda ambapo naye kwa Uongozi wake mzuri mpaka sasa anaendelea kuongozo mtaa huo na wana Mtaa uwaelezi lolote juu ya Ally Msungi.
Wiki iliyopita Mtandao huu umefanikiwa kuzungumza na Ally ambapo ameelezea A-Z alivyomshinda kaka yake ambaye wiki iliyopita alifariki dunia kwenye ajali eneo la Nane nane.
Simulizi hiyo endaendelea baadae hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

No comments:
Post a Comment