Wachezaji wa timu ya Viwawa wakipokea maeekezo kutoka kwa kpcha wao wakati wa mapunziko jana
Kikosi cha Back Viba nao wakipokea maelekezo kutka kwa kocha wao
Na Dunstan Shekidele,Morogoro,
MCHEZAJI nyota wa Mabingwa wa kihistoria Dar- Yanga Afrikani, Kibwana Shomari amenaswa na Mtandao huu akishuhudia uzinguzi wa Ligi daraja la Nne Wilaya ya Morogoro iliyoanza kutimua vumbi jana Uwanja wa Saba saba.
Kama kawaida Mtandao huu unaongoza kwa habari kali za chini ya Kapeti baada ya kumuna Kibwana ulimvaa na kumuiza kulikoni jana yuko Mji Kasoro bahari[Morogoro] wakati wenzake wapo nchini Morocco wakijiandaa kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Leo hii Leo.
Majibu yake haya hapa. “Nikweli Shekidele wenzangu wako Morocco, mimi sikusafiri natimu nimeumia kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa.
Mwandishi. Hooo Ok je kwa sasa unaendelea Je?
Kibwana. Mungu ni Mwema naendelea vizuri wenzangu wakirejea nitajiunga nao kuendelea na mazoezi ya kuipambania timu yetu.
Mwandishi. Sawa.
Ifahamike wachezaji wengi mastaa kutoka Mkoa wa Morogoro kama vile Nickson Job, Abuutwarib Msheri, Kibwana Shomari, Shomari Kapombe, Mzamiru Yassin, Dickson Kibabage, Shiza Kichuya, Salum Kihimbwa, Japhari Kibaya.
Huko waliko wanafanya kazi tu mijengo yao wameyajenga nyumbani kwao Morogoro hivyo wanapotata mapunziko mafupi au marefu fasta urejea nyumbani kwao Morogoro mijengo yao.
Pichani Kibwana Shomari[Kati] akishuhudia uzinduzi wa Ligi daraja la Nne kati Black Viba ya Vibanda kata ya Mbuyuni na Viwawa Fc kutoka Kigurunyembe Kata ya Kilakala.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali kwa muda wote wa dakika 90 timu hizo zilitoka sale ya bao 1-1,pichani kulia ni kocha msaidizi wa timu ya Moro Kids ya watoto chini ya Miaka 17 na kushoto ni kocha wa zamani wa timu ya Moro Kids Juma Micho.




No comments:
Post a Comment