Thursday, March 26, 2026

WEMA ALIOFANYA HAYATI MSUNGI KWA MLEMAVU MATAMA HUU HAPA.


Matama na mkewe wakizungumza na Mwandishi wa habari. 

Matama akitabasau na kuendelea na baishara yake baada ya kupata baiskeli mpya.
Matama akimbaidhi pesa hizo Mwenyekiti wa Mtaa kulia ni Mzee Omari Mbezi aliyetuzia kiwanja hicho.
Shekidele na Matama wakiwa kwenye Pikipiki wakienda kununua Kiwanja.
       Shekidele akimkabidhi Matama Milioni moja na Nusu
            Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

KABLA ya kutaja wema aliofanya aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Saadan Hayati Hassan Msungi kwa Ndugu yetu Mohamed Matama ambaye ni Mlemavu wa Miguu, nieleze kwa ufupi sababu za Mwenyekiti huyo kuguswa na kutoa msaada huo.

Matama anayeishi Mtaa wa  River Side Kata ya Mwembesongo jirani kabisa na Mtaa wa Saadan anaendesha Maisha yake kwa biashara ya kuuza Maji Mitaani na kwenye viwanja wa Mpira akitumia usafiri wa baiskeli.

 Takribani Miezi miwili Mwandishi wa habari hizi hajamuona Matama Mtaani wala kwenye viwanja wa Mpira jambo ambalo si kawaida yake.

  Hali hiyo ilimsukuma Mwandishi huyo  kwenda nyumbani kwake kumjulia hali na kujua kipi kinamsibu.

 Alipofika alimkuata Matama amejikunyata na Mkewe Bi Maua Said na alipoulizwa kulikoni haonekani alijibu.

“ Shekidele kwanza ubarikiwe sana kwa moyo wako wa huruma,kilichonifanya sionekani mtaani kwa muda mrefu ni Vibaka[ Mateja] wameiba miguu yangu kama unavyojua baiskeri yangu haingia ndani mlango ni mdogo  miaka yote inalala hapo Nje.

Sasa Mwezi uliopita Mateja hao wamekuja na Misumeno wameikata kata  na kwenda kuuza  vyuma chakavu kulipokucha mimi na mke wangu  tumeshuhudia mabaki ya vyuma ilituumiza sana  kwa sasa mimi na mpendwa mke wangu hatuna uwezo wa kupata laki moja na Nusu  kununua baiskeri nyingine ndio maana umeona sielewi nipo tu nyumbani” alisema Matama kwa sauti ya kinyonge.

Alipoulizwa kwa sasa anapataje pesa ya matumizi?

Alijibu.” Kukicha mke wangu anakwenda kufanya kazi ya kufua kwenye majumba ya watu akilipwa elfu 4 au 5 tunanunua chakua maisha yanaenda”

Kuptia Mwandishi wa habari hivi Mungu amefanya jambo Matama amepata baiskeri mpya kama hiyo haitoshi amenunua kiwanja na kujenga nyumba kubwa ya kisasa, nini kimetokea endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

                         


 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment