Wednesday, March 25, 2026

UCHAGUZI SERIKALI ZA MTAA FAMILIA YA MSUNGI UPINZANI WAO NI KAMA ULE WA SIMBA NA YANGA.



Kassim kushoto akipinga kauli ya Ally [kati mwenye koti] kulia ni Wazee wakifuatilia mahojiano haya.

 
                    Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 MWENDELEZO wa Stori ya Familia ya Msungi na hii imetokana na kifo cha Mpendwa wetu Mwenyekiti wa zamani wa Mtaa wa Saadan Kata ya Mwembesongo, hayati Hassan Msungi aliyefariki wiki iliyopita kwenye ajari iliyotokea Nane Nane eneo la Jordan mkoani hapa.

Jana Mtandao huu ulishia kwenye kipengele cha Mwenyekiti wa sasa wa Mtaa huo Ally Msungi ambaye alinyakua kiti hicho kwa leseni ya CCM baada ya kumbwaga kaka yake,Hayati Hassan Msungi aliyeongoza mtaa huo kwa vipindi viwili kwa leseni ya Chama cha Wananchi CUF toka Mwaka 2009 mpaka 20014.

 

Kwenye uchaguzi  wa Mwaka 20019 CCM Kata ya Mwembesongo waliamua kumteua Ally Msungi kupambana na kaka yake.

Wiki iliyopita baada ya mazishi ya Hassan Msungi Mwandishi wa habari hivi alimtaka Ally  kueleza namna alivyomshinda kaka yake aliyekuwa kipenzi cha wana Mtaa huo.

                 MSIKIE ANACHOSEMA.

“ Kila kitu ni kwa zamu kaka  baada ya kuongoza  wa vipindi viwili, uchaguzi wa 2019 niliamua kuingiza timu  kupambana naye nikipeperusha bendera ya chama dume  CCM”Alisema Msungi na kuongeza.

“Mwisho wa siku nilimshinda  mpaka sasa naendelea kuongoza mtaa ambapo uchaguzi wa mwaka juzi 2024 nilishinda tena kwa kishindo”alimalizia kusema.

Hata hivyo Kauli hiyo ilipingwa vikali na Kassim ambaye ni mdogo wao wa mwisho.

“ Sio kweli Shekidele kumbuka uchaguzi wa 2019 wagombea wengi akiwemo kaka Hassan walieguliwa ndipo huyu kaka Ally alipopata nafasi ya kupita bila kupingwa wangeingia wote kwenye sanduku la kura kaka Ally ungepigwa asubuhi na mapema”alisema

 

Mtandao huu ulipomuliza Ally ni kweli alivyosema Mdogo wake  alijibu.

“ Ni kweli lakini kabla ya kaka kuegeliwa kilipigwa kwenye kampeni za awari za nyumba kwa nyumba labla hayati kaka yangu kueguliwa na tume ya uchaguzi”Alisema Ally huku akiangua kicheko.

Mwandishi. Hebu tueleze siku mlivyokabidhiana ofisi ilikuwa je?

 

Ally. Haa Shekidele siunajua kaka yangu dini ilimkaa sana kiukweli alinikabidhi ofisi vizuri na nikili kwenye uongozi wangu pale nilipokwama nilimfuata na alinipaushirikiano mzuri sana.

 

Mtandao huu ni shuhuda Ally[Pichani aliyekaa] amefuata nyayo za kaka yake ambapo kwa sasa wananchi wa Mtaa wa Saadani huwaambi kitu juu ya utendaji mzuri wa  Mwenyekiti wao huyo.

Baadae tutamalizi stori hii kwa kueleza wema aliofanya hayati Msungi[Pichani aliyesimama] wakati Mwandishi wa habari hizi alipoendesha harambee ya kumjengea nyumba Mlemavu wa Miguu Mohamed Matama.

                         


No comments:

Post a Comment