Tuesday, March 17, 2026

VITI VYA UWANJA WA MKAPA VYA HAMISHIWA UWANJA WA JAMHURI MORO.






          Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

VITI vya Uwanja wa Mkapa uliopo Kata ya M  gulani Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaamu, Vimehamishiwa Uwanja wa Jamhuri Uliopo Kata ya Boma Mkoani Morogoro.

 

Juzi Mwandishi wa habari hizi alitinga uwanja wa Jamhuri kushuhudia mchezo wa Ligi daraja la Pili kati ya Moro Kids dhidi ya Magnet Fc, gemu hiyo ilitamatika kwa wenyeji  kuendelea kufanya vibaya kwenye uwanja wao wa nyumbani baada ya kulazimiswa sale ya 0-0 na Magnet Fc.

 

 Ndani ya uwanja huo Mtandao huu ulishuhudia lundo la viti vyenye rangi ya Oranger na Bluu ndani ya uwanja hau unaomilikiwa na Chama cha Mapinduzi’CCM’.

 

 Mwandishi wa habari hizi aliingia kazini ambapo alimtafuta meneja wa Uwanja huo John Simkoko ambapo alipoulizwa kuhusiana na viti hivyo alijibu hivi.

 

“ Shekidele Mimi kama meneja nimepokea viti 3500 vile pale lakini  maelezo zaidi mtafute Katibu Mkuu wa chama cha Soka Mkoa wa Morogoro yeye ndiye aliyenikabidhi viti hivi”alisema Mzee Simkoko ambaye ni kocha wa zamani wa timu za Reli ya Morogoro, Mtibwa Sugar na timu ya Taifa ya Tanzania.

 

Akizungumza kwa njia ya simu na Mtandao huu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Morogoro’MRFA’Alfred Mdende Maarufu Mteule alisema.

 

“Kama unavyojua Uwanja wa Mkapa kwa sasa unafanyiwa matengenezo makubwa ikiwa ni maandalizi ya Michuano ya Mataifa ya Afrika ‘AFCON’ yatakatofanyika mwaka 2027 nchi  za Tanzania, Kenya na Uganda.

 

Hivyo viti vya zamani zilivyotolewa   tumepewa sisi wa Morogoro, awamu ya kwanza tumekabidhiwa viti 3500 tunategemea kupewa vingine 3000”alisema Mteule na kuongeza.

“Shekidele kama umefika ndani ya uwanja wetu wa Jamhuri utashuhudia jukwa la wageni rasmi tumeweka sampo ya  mstari mmoja tukihitaji mtu tutakayempa kazi afunge viti kwa mfumo huo”alisema Katibu huyo.

 

Alipoulizwa mkandarasi wa kuweka viti hivyo wameshampata? Alijibu.

 

 “Swari zuri  Shekidele  kuna fundi mmoja amenipa Qoutation zake natafuta wengine ili niangalie unafuu uko wapi lengo letu kuweka viti  6000 kwenye majukwa mawili yale ya Simba na Yanga, baadae tutamalizia majukwa ya mzunguko upale ule ambao hauna bati”alisema Mteule.

No comments:

Post a Comment