Monday, March 30, 2026

A-Z UJENZI NYUMBA YA MLEMAVU MATAMA SEHEMU YA MWISHO.

Matama akimshukuru Mungu huku akimuombea Dua Shekidele Kwa kumsimamia Kwenye jambo lake.
 Matama akilipia kiwanja kwa Mwenyekiti wa Mtaa kulia ni muuzaji wa kiwanja hich Mzee Omar Mbezi

Bi Maua Said mke wa Matama naye aishiriki kusomba maji na kujaza kwenye pipa tayari kuanza ujenzi wa Msingi
                       Matama akiwa mbeke ya mjengo wake
lnjinia hayati Mzee Hussein na msaidizi wake wakichra ramani ya nyuma ya Matama
Matama akishuhudia hayati Mzee Hussein akichora ramani ya nyumba yake
                                         .....Shekidele akichimba msingi
                                               ......Matama akitoa udongo
                                Mungu ni mwema.nyumba imepauliwa
   Injinia  Hayati Mzee Hussein amekamilisha ujenzi wa msingi

                      ......Matama akiwa nje ya nyumba yake
Nyumba iliyojengwa na watu wa Mungu wadau wa Mtandao Pendwa wa Shekidee yenye nyumba 3 sebure,Jiko imekamiika hii hapa Mtanda huu unawashukuru watu wote walioguswa na changamot za ndugu yetu Matama na kuamua kuta michango iliyofanikisha kukamilika kwa nyumba hii
 
                  Na Dunstan Shekidele,Morogoro
NAFUNGA stori hii ya kumbukizi ya Ujenzi wa nyumba ya Mlemavu Mohamed Matama kwa kuwashukuru wote walioisikia sauti ya Mungu na kuniunga mkono kwenye jambo hili.
 
Kipekee niwashukuru wadau wote wa Mtandao Pendwa wa Shekidele pande zote za dunia ambapo wengi wao walituma pesa kutoka nje ya nchini na ndani ya nchini wakichangia ujenzi huo.
 
Pia navishukuru vyombo vya habari vilivyoniunga mkono kwenye harambee ya ujenzi wa nyumba hiyo, vyombo hivyo ni Global Publishers, TBC Taifa na Abood Media ambayo kupitia kipindi kilichokuwa kikiongozwa na Zuberi Mkalaboko walimuita Matama studio na kufanya naye mahojiano Live. 
 
      HAYATI MZEE HUSSEIN MUNGU AKUBARIKI.
 
Baada ya kuona ninavyopambana na ujenzi huo, lnjinia Mzee Hussein ambaye kwa sasa ni marehemu alinifuata na kunieleza hivi.
 
“ Shekidele nimeona unavyompambani ule Mlemavu Munngu atakubariki nami kama fundi nitakusapoti kwenye jambo hilo nitachora ramani na kujenga msingi bure ninachokuomba ni nauli kutunulia chakula mimi na msaidizi wangu na kutafuta vijana wa kuchimba msingi”alisema hayati Mzee Hussein pichani mwenye kofia.
 
Mwandishi wa habari hizi alimshukuru Mzee huyo na kutekeleza maagizo hayo, hilo la kuchimba msingi tulikosa pesa kwa wakati huo hivyo Shekidele na Mlemavu huyo walifanya kazi hiyo huku mke wa Matama Bi Mau Said akifanya kazi ya kusombelea maji.
 
Mungu Mkubwa ndani ya Mwaka mmoja tulipata pesa ya kununua kiwanja na kukamilisha nyumbani hiyo ambapo kwa sasa Mpendwa wetu Matama anaishi na mkewe huku chumba chao kikiwa na choo ndani[Master]
 
Juzi nilifika kwenye nyumba hiyo iliyopo kata ya Kichangani jirani na Karakana kuu ya Reli nikakutana na Mzee Omari Mbezi aliyetuuzi kiwanja hicho akisema.
 
“ Shekidele ubarikiwe sana kwa sasa sisi majirani wa Matama tunafura kubwa kila siku mpira tunaangalia bure nyumbani kwake nyakati za usiku watoto wetu wanakwenda kuongalia Filamu zinazirushwa Azam Two”
 
Mtandao huu unawashukuru wote waliochangia ujenzi wa nyumba hii malipo yenu mtayakuta kesho kwa Mungu namini hakuna mtu aliyefirisika kwa kumsaidia mwenye uhitaji. 
 
Nakili kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu kwenye ujenzi wa nyumba hii sikutoa hata senti tano vitu nilivyotoa ni Taaruma yangu ya Uandishi wa habari, Nguvu zangu, vifaa vya ujenzi kama vile mapita ya maji na mbao za Linter, Muda wa mwaka mzima wa usimamizi wa nyumba hii na mafuta ya pikipiki kuzunguza mitaani Mwaka mzima. 
 
Ninachojivuni ni kwamba nimekamilisha kazi niliyotumwa na Mungu na nimeweka alama ya kuwa Mwandishi pekee Tanzania niliyetumia kazi yangu ya Undishi wa habari kumjengea nyumba ya kisasa Mlemavu Matama pichani anayemuombe dua Mwandishi wa habari hizi

No comments:

Post a Comment