Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
MSANII Staa wa nyimbo za lnjiri nchini Bahati Bukuku amehubiri kupitia wimbo akisema ‘Dunia haina huruma’.
Kweli kuna baadhi ya watu hapa duniani hawana huruma, wakati Mwandishi wa habari hizi akipambana kusaka pesa za kumjengea nyumba Mohamed Matama ambaye ni Mlemavu wa Miguu.
Matapeli wametumia fursa hiyo kumtapete mlemavu huyo elfu 50 alizopewa msaada na aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro’RPC’ SACP Urlch Matei.
PICHA HILO LILIKUWA HIVI.
Mbali na kuendesha harambee kwenye Mtandao Pendwa wa Shekidele,Mwanahabari huyo pia alizungunza na Mlemavu huyo kwa viongozi na na Mtajiri wa Mkoa wa Morogoro kuomba msaada.
Dunstana Shekidele na Matama walitinga Ofisi wa RPC Matei Ghorofa ya kwanza kwa kuwa Ghorofa hilo halina lifti Mlemavu huyo kwa Ujasiri alitambaa na kupanda ngazi mpaka juu ya ghorofa hilo.
Mungu ambariki sana RPC Matei tulipofika tu ofisini kabla ya kumueleza shinda yetu RPC huyo alisema
” Du huyu jamaa kapandaje ngazi shekidele ungenipigia simu nije huko chini tuzungumze mbona kuna ofisi nyingi kuliko kumpa adhabu ndugu yetu huyo ya kupanda huku”
Mwanahabri huyo alimuomba msamaha ‘Big Bos’ huyo wa Polisi Mkoa Morogoro na Moja kwa Moja alimueleza shida za Mlemavu huyo ambapo RPC Matei aliguswa na kumkabidhi Msaada wa elfu 50 huku akisema
“ Shekidele ubarikiwe sana kwa kazi hii unayoifanya kwa sasa ninakiasi hichi kidogo naomba mkipokee mwisho wa mwenzi nitachangia kiasi kingine “alisema RPC huyo.
Kabla hayatimiza ahadi yake hiyo RPC Matei halihamishiwa Mkoa wa Mbeya, Mtandao huu unazidi kumuombe baraka nyingi na wote waliochangia ujenzi wa nyumba hiyo. UTAPELI SASA.
Matama ni muunini wa dini ya kiislamu aliyejaliwa kuswali swala 5 hivyo wakati tunatoka Polisi muda wa kwenda Msikiti ulifika.
Baada ya kutoka Msikiti njini alikutana na Matapeli wanaofuatilia habari za harambee ya ujenzi wa nyumba yake kwenye Mtandao wa Shekidele, Magazeti na Redio.
Matapeli hao wakamsimamisha na kumueleza hivi.
“Tunaona Shekidele anakupambani sana bosi wetu ameona habari zako hivyo ametutuma tukutafute akuchangie mabati na Cement sasa kama una lakini moja tupe tukodi gari sasa hivi twende na wewe ukavibebe vitu vyako”
Matama aliwaambia kwa muda huo alikuwa na elfu 50 tu Matapeli hao wakajifanya kumpigia simu bosi wao, baada ya kukata simu hiyo ya uongo wakamueleza Matama kwamba bosi wao ametuma elfu 50 hivyo awape hiyo 50 waende kwa wakala wakatoe wakodi gari wampitie waende kuchukua vifaa hivyo.
Matama amezama msukoni na kuwakabidhi pesa, wajomba wamelala mbele wakimuacha matama akiendelea kusubiri kwa zaidi ya masaa 2 bila mafaniko.
Ndipo alipoamua kumpigia simu Shekidele huku akiangua kilio Mwanahabri huyo alipofika awari alibeba jukumu la kumbembeleza na kumueleza maeneo ya faraja aliokaa sawa nikamruhusu erejee nyumbani tuonane kesho.



No comments:
Post a Comment