Friday, February 27, 2026

HABARI KALI YA KIJAMII WIKI HII NI HAKI MTOTO MCHANGA KUNYWA DAWA HUKU ANA NYONYA MAZIWA YA MAMA?


                    Dr Sadick akizungumza na Mtandao huu


                 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

IMEZOELEKA kitabibu Mtu anapougua na kupewa dozi ya dawa, hushauri na daktari asinywe maziwa mpaka atakapomalizi dozi.

 

Hali hii imeonekana kuwa tofauti kwa kundi la watoto wachanga ambapo utafiti wa awari uliofanywa na Mwandishi wa habari hizi umebaini watoto wengi wachanga ambao chakula cha kikuu ni Maziwa ya Mama wanapougua hupewa dozi za dawa huku wakiendelea kunyonya maziwa ya mama zao.

 

Wiki iliyopita Mwandishi wa habari hizi akiwa kwenye kikao cha kikundi mfla cha ‘kikobe’alimshuhudia Mwanamke mmoja mwanakikundi akimpa dawa Mtoto wake mchanga.

 

Baada ya kumnywesha dawa hiyo Mtoto huyo alianza kuangua kilio kwa uchungu wa dawa, hivyo Mama huyo aliamua kumnyamazisha  kwa kumnyonyesha.

 

Kufuatia hali hiyo Mtandao huu alimuliza Mama huyo iweje amempa dawa mtoto na Muda huo huo ana mpa maziwa?

 

Mama huyo alijibu.”Watoto wachanga mara nyingi wanaugua mara kwa mara na chakula chao kikuu ni haya maziwa yetu binafsi Clinc sijashauriwa kuacha kumnyonyesha mtoto pale ninapompa dawa” alisema Mama huyo ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sababu maalumu.

 

Kufuatia majibu hayo Mwandishi wa habari hizi jana aliamua kumtafuta Daktari kwa lengo la kutapa majawabu ya jambo hili huyo hapa Daktari Sadick Juma.

“ Swali zuri sana iko hivi kwa ukuu wa Mungu Maziwa ya Mama nitofauti na Maziwa mengine Maziwa ya binadamu yana Virutubisho na Kinga hivyo Maziwa hayo hayauwi nguvu ya dawa ili kuthibitisha hilo ndio maana mama anapokuwa na maradhi ya kuambukizi huwa tunamshauri asimnyonyeshe mtoto”alisema Dr Sadick  na kuongeza.

 

Kweli huwa tunashauri kwa mtu mzima au mtoto wa umri wowote anapomeza aina ya daiwa asitumie maziwa ya wanyama kwa sababu dawa nyingi zina Hasid hivyo maziwa hayo huuwa nguvu ya dawa.

 

Katika kuongezea hilo sumu nyingi zina Hasid tumeshuhudia mara  kadhaa mtu akinywa Sumu akiwahiswa kupewa Maziwa anapo hii ni kwa sababu Sumu nyingi zina Hasid hivyo zikikutana na Maziwa zina zina kosa nguvu.

 

Ila kuna dawa nyingine hazina Hasid kama vile Mseto unaweza kumeza huku unakunywa maziwa haina shida yoyote”alisema Daktari huyo kutoka hospital ya Wahindi ya Ahhamadiya iliyopo katikati ya Mji wa Morogoro.  

                  


 

 

No comments:

Post a Comment