Wednesday, January 21, 2026

LOVE IS A POLSON.[KUPENDA NI SUMU]










 

   

HUENDA kuna ukweli kwamba kupenda kitu au Mtu ni kama sumu,

 

Ligi ya Mabingwa barani Ulaya imeendelea jana usiku huku mashabiki wengi duniani wakitupia jicho gemu kubwa ya Inter Milano ya Italia na Arsenal ya England.

 

Kwa saa za Tanzania gemu hiyo ilianza majira ya saa 5 usiku na kutamatika saa 7, kwa mapenzi ya mchezo wa Soka mashabiki wengi waliamua kukesha kuangalia gemu hiyo iliyotamatika kwa chama bora duniani kwa sasa Arsenal washika bunduki wa jiji la Maraha la London kuwanyuka wenyeji wao kwa chuma 3-1.

 

Miongoni mwa mashabiki hao ni shabiki ‘lia lia’ wa Arsenal  Dunstan Shekidele’Ez Come Ez Go’ alikesha na kikombe cha kahawa akicheki gemu hiyo kwenye Hotel ya Glonency iliyopo Nane Nane Kando kando ya barabara kuu ya Morogoro-Dar –es-salaam jirani kabisa na uwanja wa maonyesho ya wakulima Nane nane Kanda ya Mashariki.

 

pIchani Shekidele aliyetinga jezi Mpya ya Arsenal akimshuhudia mshambuliaji wa Arsenal Gabril Jesus akipachika mabao 2 kwenye ushindi huo wa bao 3,

 

lfahamike Jesus ambaye ni Raia wa Brazil kwa kipindi kirefu alikuwa nje ya uwanjani akiuguza majeraja kwa sasa amerejea na Moto wake ule ule.

 

Mpiga picha wa Mtandao huu akitumia kamera ya kisasa alifanikiwa kunasa magori hayo 2 kwenye Luninga kubwa ya hotel hiyo kama anavyoonekana pichani Jesus jezi namba 9 akimtungua mara 2 kipa wa lnter Milano.

 

No comments:

Post a Comment