Sunday, January 25, 2026

FAINALI ZA AFCON 2025.KAULI YA SADIO MANE NI YA KIUNGWANA.

Sanamu lenye mfano wa Sadio Mane limejengwa nchini kwao Senegal
......Mane akipongezwa na wenzake huku wakimtwisha kombe kichwani
                               Mane akiwa na familia yake


Na Dunstan Shekidele.Morogoro.

FAINALI za Mataifa ya Afrika'AFCON' zilizoanza kutimua vumbi nchini Morocco  Disemba 21 na kutamatika January 18 kwa Senegal kutwaa ubingwa akiwanyuka  wenyeji Morocco kwa bao 1-0.

 Morocco walijikuta wakitoka uwanjani vichwa chini huku wengine wakimwaga machozi kwa uchungu wa kulikosa kombe ndani ya ardh yao ya nyumbani.

Wachezaji wengi wa Morocco walitinga uwanjani na familia zao  kwa lengo la  kupiga picha nazo wakiwa na kombe hilo.

Hali ilibadilika walijikuta wakiwa shuhudia wachezaji wa Senegal wakinyakua mwali huyo na kupiga naye picha na familia zao huku wachezaji wa Morocco wakienda nunia kwao baada ya kuwanyiwa ubaya na ubwela na Senegal ya Sadio  ‘Pesa’ Mane

Mara baada sherehe hizo kutamatiza Nahodha wa Senegal Mstaarabu Sadio Mane alizungumza na waandishi wa habari.

Kwenye mazungumzo hayo Mane. Pichani na familia yake alisema maneno yaliyojaa hekima,Utu na busara.

"Huu ushindi ni wa Waafrika wote waliokuwa wakituunga mkono"

Mwafrika kutoka Afrika Mashariki na Kati nchi Pendwa ya Tanzania Dustan Shekidele alikuwa mmoja wapo aliyeiunga mkono Senegal kwenye Fainali hiyo uku akiiombea mabaya Morocco wafungwe.

Kama lpo lpo na riziki ya mtu haizuiwa bali inacheleweshwa tu, licha ya refa Mkongo Man kuonyesha dhairi kuibeba Morocco kiasi cha Kocha wa Senegal kuamua kususia mchezo huo baada ya refa huyo kuipa Pelnaty Morocco dakiza za mwisho mwisho za mchezo huo.

Hata hivyo Sadio Mane aliyebaki peke yake uwanja baada ya wenzake 10 kususi mchezo huo na kutoka uwanjani wakikimbilia vumbani.

Mane aliwafuata wenzake na kuwasihi warejee uwanjani.wachezaji hao walimtii Nahodha wao huyo na kurejea uwanjani baada ya gemu hiyo kusimama kwa takribani dakika 10.

Waliporejeja zikiwa zimesalia takribani dakika 7 mchezo huo kutamatika Morocco walipiga ichani hiyo ambapo kw amshanga wawengi mchezo wa Morocco alipiga kishuti ‘Mtoto’ kilichodakwa na kipa wa Senegal Mendy.

Dakiza za magharibi ya roho zakika za mwisho Mwamba Sadio Mane alifunga bao lililodumu hadi mwisho wa mchezo.

 

Ikumbukwe  fainali za kombe la Dunia zilizofanyika nchini Qatar mwaka 2022 na wawakishiri wa bara la Afrika Morocco kuweka rekodi ya kutinga Nusu fainali ya michuano hiyo.

Kocha mkuu ww Morocco akizungumza.na waandishi wa habari alisema.

Mafanikio hayo waliyotapata ni kwa wananchi wa Morocco na sio kwa wafrika.

Kauli hiyo ilizua mjadala mzito barani Afrika.kufuatia hali hiyo uongozi wa juu wa Morocco ulijitokeza hadharani na kupinga kauli hiyo.

Ukikanusha maneno hayo ya kocha wao uongozi huo ulisema kauli hiyo si ya wana Morocco bali ni kauri binafsi ya kocha.

Maneno hayo yalipunguza   machungu ya waafrika wengi waliokuwa wakiisapoti timu hiyo kwenye michuano hiyo mikubwa duniani.


 

No comments:

Post a Comment