“ Ee bwana tunakuja mbele yako na Moyo wa shukrani, kupitia maandiko yako umetamka bayana kwamba Yule atakayekushukuru kwa wema uliomfanyia utamzidishia mara dufu.
Asante kwa Wiki hii nyingine ya kuishi,tupoanza wiki hii mpya.tunaomba tupenguvu ujasiri na Upendo wako na utiririke ndani yatu,ukigusa maisha ya wote tutakao kutana nao wiki hii mpya inayoanza kesho jumatatu.
Kipekee tunakuomba si kwa kukulazimisha bali kwa utashi wako, waponye wagongwa waliolazwa mahospitalini na wale wa wanaojiuguza majumbani.
Aidha tunakuomba uwapefaraja ya kweli watu wote wanaopitia changamoto mbali mbali ambao tumaini lao wamelielekeza wewe Muumba wa mbingu na Ardhi usiyefananishwa wala kulinganishwa na kitu chochote.
Wee Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema tunainmgia kwemnye miyezi ya toba, Kwarezima kwa wakristo na Ramadhani kwa Waislamu tunakuomba tufanyie wepesi vile vile utuepushe na maradhi, Vishawizi kibaya na hira mbaya ili tuingia kwenye funga zetu tukiiwa wasafi wa Moyo na Mwili.
Wote tunaoamini na kuguswa na sala na dua hii tuseme AMENI”.

No comments:
Post a Comment