Thursday, February 5, 2026

DIWANI AFUNGUKA ALIVYOPIGIWA SIMU NA HAYATI MZEE HOOD.

                            Mzee Hood enzi za Uhai wake

 Mwandishi wa habari hizi[kati]akizungumza na Mhe Malingo pichani kulia

 

Kushoto anayefuatia kwa makini mahojiano hayo ni  Mhe Abdallah Ally Meya diwani wa zamani wa kata ya Chamwino ambaye pia kwenye uchaguzi uliopita naye kura hazikutosha kwenye mchakato wa Kura za Maoni ndani ya chama chao cha CCM

               

                    Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

MWENDELEZO wa Story ya kifo cha tajiri wa mabasi Mkoani Morogoro, hayati Mzee Mohamed Hood Said[90]ambapo jana tuliishia kwenye maelezo ya  Diwani wa Kata ya Mji Mkuu Mhe Hassan Malingo ambaye aliombwa na Mzee Hood kumpokea kwenye nafasi hiyo ya udiwani ndani ya kata hiyo iliyopo katikati ya Mji wa Morogoro.

 

Sasa tuendelee na maelezo ya Mhe Malingo “Nilipotoka Mwanza na kufika Morogoro nilimueleza bosi Merey ambaye aliniruhusua kuingia kwenye ulingo wa siasa.

 

Nikamjuisha Mzee Hood akaniita ofisini kwake pale Mtawara kwenye gereji yake ya mabasi,baada ya mazungumzo marefu akaniambia nimuone mtu mmoja anayeitwa Kunga nilipomuona jamaa huyo kumbe walishanichukulia fomu ya kugombea udiwani nikaijaza na kuingia kwenye kinyang’anyiro”alisema Mhe Malingo na kuongeza.

 

“ Kwa bahati kwenye uchaguzi huo wa Mwaka 2005 nilishinda na nilidumu kwenye naafasi hiyo kwa miaka 20 baada ya uchaguzi wa Octobar mwaka jana kushindwa kwenye kura za maoni ndani ya chama chetu”alimalizia kusema Mhe Malingo.

 

Katika uchaguzi mkuu uliofanyi8ka Octobar 29 Mwaka jana Khalid Matengo alishinda udiwani katika kata hiyo ya Mji Mkuu inayotajwa kuwa kata tajiri ndani ya jimbo la Morogoro lenye kata 29.

 Wachunguzi hao wa mambo wanadai kata inayofuata kwa utajiri ni kata ya Mafisa ambayo ndani ya kata hiyo kuna viwanda 10 na Stend ya Mabasi ya Msamvu.

 

Baada ya kushinda Udiwania Matengo mwenye Elimu ya Chuo Kikuu aligombea Umeya na kufanikiwa kushinda ambapo kwa sasa ‘Mwana wa Pakaya’ huyo Mpogoro wa Ifakara ndiye ‘Big Bos’ wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

 

Ifahameka  Mwaka 2000 baada ya kushinda Udiwania wa kata hiyo Mzee Hood aligombea Umeya lakini kwa bahati mbaya kura hazikutoka.

           



No comments:

Post a Comment