Mwenyekiti Kamanga akiwa na Mjumbe wake Jastini Sanga Sammy aliyeketi
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
KAMA kawaida kila wiki Mwandishi wa Mtandao huu husaka habari kali ya kitaa na kuirusha hewani.
Tunakumbuka mwezi uliopita ulifanyika uchaguzi wa Viongozi wa serikali za Vijiji, Vitongoji na Mitaa kwa kushirikisha vyama vyote vya siasa.
Kwa upande wa Jimbo la Morogoro Mjini lenye Kata 29 na Mitaa 294 CCM wameshinda Mitaa 293 huku Chadema wakinyakua mtaa mmoja wa Lukobe Juu Kata ya Lukobe.
Kwa matokeo hayo Mwandishi wa habari hizi ilimsukuma kupiga gia Pikipiki hadi Mtaa huo na kufanya mahojiano Maalumu na Mwenyekiti huyo kwa lengo kusikia kauli yake juu ushindi na namna anavyofanya kazi na wajumbe mtaa wote 5 kutoka CCM.
Mahojiano yetu ndani ya ofisi ya mtaa yalikuwa hivi.
Mwandishi. Kiongozi hongera kwa ushindi, awari ya yote tukufahamu kwa majina yako chama unachotoka na Mtaa unaouongoza.
Mwenyekiti. Asante kwa pongezi,lakini kabla ya kijitambulisha kwa niaba ya wajumbe wangu wa Mtaa nikushukuru kwa kuwa Mwandishi wa habari wa kwanza kuja kutuhoji toka tulivyoibuka washindi.
Kwa majina Naitwa Joseph John Kamanga ni Mwenyekiti wa mtaa wa Lukobe Juu Kata ya Lukobe.kupitia chama changu pendwa cha Chadema.
Mwandishi. Tupe histori fupi ya maisha yako ya kisiasa na sera ulizotumia kwenye mikutano ya kampeni na wananchi kukuelewa.
Mwenyekiti. Ok awari nilikuwa chama cha TLP chini ya hayati Agostino Lyatonga Mrema kwenye uchanguzi wa serikali za Mtaa Mwaka 2009 - 2014 niliibuka mshindi kiwawashinda wagombea wa CCM na Chadema.
Uchaguzi wa Mwaka 2014-2019 nilihama TLP na kujiunga na Chadema kwenye uchaguzi huo pia nilishinda.
Uchaguzi wa 2019-2024 nilieguliwa na mamlaka za uchaguzi kwa madai ya kukosa sifa.
Uchaguzi wa 2024-2029 licha ya kuegeuliwa uchaguzi uliopita lakini wananchi wa taa huu walikumbuka utendaji wangu juzi wamenichagua tena .
Siri ya ushindi wangu ni kutatua kero kwa vitendo wananchi wa mtaa huu wanalijua hilo.
Wewe mwenyenye nishahidi Decemba 8 tuliwasiliana uje kunihoji nilikwambia niko bize site kwenye matatizo ya wananchi wangu ambao baadhi yao waliadhirika na ile mvua kubwa ya tarehe 8.
Siku zote kwenye matatizo ya wananchi wangu situmi mtu nakwenda mwenyewe ili ikitokea nimeulizwa nielezelee kitu nilichokiona na sio cha kuambiwa.
Mwandishi. kwenye ushindi huo wajumbe wako wanatoka chama gani na majina yao.
Mwenyekiti. Wajumbe wote 5 wanatoka CCM ambao ni Asha Hamisi,Rosemary Charles, Fred Alfred, Jastin Sanga Sammy na Mohamed Nyenje.
Mwandishi. kama hivyo ndivyo je ufanisi wenu wa kazi uko je hasa mkizingatia mnatoka vyama tofauti?
Mwenyekiti. Swali zuri kabla ya kuanza kazi tulipewa semina elekezi na Afisa Mtenda wa Kata Bi,Mariam Rajab, lakini cha kushangaza mmoja wawajumbe wangu Mohamed aligoma kufanya kazi na mimi.
Kufuatia hali hiyo aliketishwa chini kaelezwa nashukuru kwa sasa nafanya naye kazi vizuri namtuma kazi anafanya.
Mwandishi. Mwisho unalipi la kuwaeleza wajumbe wako na wananchi wa mtaa wa Lukobe juu.
Mwenyekiti. Kwa upande wa wajumbe wangu toka tulivyoapishwa November 28 na kuanza kazi November 29 nafanya nao kazi vizuri binafsi sina kinyongo nao labda kama wao wanakinyongo na mimi.
Kuhusu wananchi nawambia asante sana kwa kutuchagua mimi na wajumbe wangu kilichobaki kwetu ni kuwatumikia kwa weledi kwenye kindi hichi cha miaka 5 waliotupa.
Mwandishi. Umekili umetoka chama cha upinzania na umetangazwa mshindi, je unawambia nini baadhi ya wagombea walioshindwa na kudai wameibiwa kura?
Mwenyekiti. Swali hilo siwezi kulijibu kwa undani lakini itoshe kusema mimi nimeshindwa kwa nguvu ya umma ya wananchi wangu ambao walionyesha ushirikiano mkubwa toka zoezi la upigaji kura mpaka hatua ya kutangazwa matokeo.
Mwandishi Asante sana kwa ushirikiano wako kiwani na swali lolote nitakupigia simu.
Mwenyekiti. Asante na karibu wakati wowote.
Baada ya kuzungumza na mwenyekiti Mwanahabari huyo aliyevuka kata 6 hadi kufika kata hiyo ya Lukoba iliyopo pembezoni mwa Mji wa Morogoro alizungumza na mmoja wawajumbe hao ili kuwasikia nao wanalipi la kusema.
Moja ya kauli ya mjumbe huyo ni Malalamiko yake kwa mwenyekiti kuzunguka na Muhuri mfukoni kwake, habari hii itaruka hewani hivi punde hivyo.
No comments:
Post a Comment