Chikolla akimkabidhi moja wa Tuzo Profesa Madundo ambaye ndiye mmiliki wa taasisi ya Moro Kids.
Ishu ya Tuzo Chikolla alianza kunyakua toka akiwa mdogo, pichani akinyanyua Tuzo baada ya kukabidhiwa na mmoja wa mawazi baada ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya Ligi ya Watoto.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
MUUAJI wa Yanga Winga hatari wa Tabora United Offen Francis Chikolla amefunguka mazito baada ya kufanya vizuri Mwezi 11 na kukabidhiwa Tuzo ya mchezaji bora wa Mwezi November na Kamati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania’TFF’.
Mbali na kukabidhi Tuzo hiyo Chikolla Mkazi wa Kididimo Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine’SUA’ Morogoro alikiwasha vilivyo mwezi huo wa 11 na kufanikiwa kunyakua uchezaji bora wa mechi mbili mfurulizo.
Gemu hizo ni ile ya Yanga ambayo wazee hao wa Supu aliangukia poa kwa kunyukwa bao 3-1 huku Chikolla akifunga bao 2,na kuibuka Man Of the Match.huku Mastaa wa Yanga kutoa mataifa makubwa wakimkodolea Macho Play huyo kutoka Mji Kasoro Bahari akipokea Tuzo hiyo.
Kama hiyo haitoshi zao hilo kutoka Moro Kids gemu dhidi KMC ambayo Nyuki hao wa Tabora wakiibuka na ushindi wa bao 2-0 Chikola alifunga bao la pili huku bao la kwanza likifungwa na Yacouba Sogne Raia wa Bukibafaso zikiwa zimesalia kama dakika 10 gemu hiyo kutamatika ilisikika sauti ikimtangaza Chikolla kuwa Man Of the March.
Hadi sasa Chikolla anamabao 4 kwenye Ligi hiyo anayeongoza kwa sasa kwa ufungani ni Seleman Mwalimu wa Fountaine Get mwenye mabao 6 .
Kufuatia mafaniko hayo jana Jioni Mwandishi wa habari hizi aliamua kumtwangia simu Chikolla na mazungumzo hayo yalikuwa hivi.
Mwandishi. Mambo vp, unazungumza na Dustan Shekidele.
Chikolla. Hooo safi sana Kaka habari za hapo nyumbani Morogoro.
Mwandishi. Safi hongera kwa mafaniko uliyoyapata mwenzi wa 11 ama kwa hakika unaipeperusha vyema bendera ya Morogoro.
Chikolla. Asante sana
Mwandishi. Leo mchana nilifika nyumbani kwenu kwa lengo la kuzungumza na wazazi wako, kusikia kauli yao juu ya mafanio yako kisoka lakini kwa bahati mbaya sijawakuta.
Chikolla. Ni kweli hawapo wamesafari kwenye majukumu ya utafutaji baba yuko lfakara na Mama yuko Turiani.
Mwandishi. Ok nilifika pia SUA kwa baba yako Mlezi wa Soka Professa Madundo Mtambo.
Chikolla. Safi sana moja ya Tuzo hizo wa Man Of the Metch nilipotoka Dar nimepita hapo nyumbani nimemkabidhi Prof Madundo huyo ndio kila kitu kwangu kwenye mafaniko ya soka.
Mwandishi. Ushauri wangu kwako endelea kukaza buti uzije ukabweteka na haya mafanikio madogo uliyoyapata achana na starehe endelea kufanya mazoezi kwa bidii utafika mbali, kwa uwezo unaendelea kuuonyesha kikosi cha Taifa kitakapo tajwa nahisi jina lako halitakosekana.
Chikolla. Asante kwa ushauri mzuri nitauzingatia na nikija Moro nitakutafuta ngoja nisevu hii namba yako.
Mwandishi. Sawa nisalimie wana Morogoro wengine hapo Tabora akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa Tabora United Rafiki Yangu Yusuf Kitumbo ambaye kwa sasa anatumikia adhabu ya kufungiwa na TFF.
Pia msalimie mwenyekiti wa sasa wa Tabora United ambaye pia ni Mwana Morogoro RCP Richard wambiye Shekidele anawasalimia sanaa.
Chikolla ok nitawafikishia salama hizo.



No comments:
Post a Comment